Serikali yaanza kutoa vifaa huduma za dharura, wagonjwa mahututi

NA OR-TAMISEMI

BAADA ya Serikali kukamilisha ujenzi wa Majengo ya Kutoa Huduma za Dharura (EMD) 80 pamoja na majengo ya kutoa huduma za wagonjwa mahututi 27 sasa vifaa vimeanza kuwasili kwenye majengo hayo.

Katika Halmashauri ya Mji Nzega mkoani Tabora wamepokea vifaa vya ajili ya kutoa huduma katika jengo la wagonjwa mahututi.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Nzega, Dkt.Jabir Juma Msuni amesema, shilingi milioni 300 zimetumika kukamilisha jengo hilo muhimu ambalo litasaidia kuongeza ubora wa huduma za dharura katika wilaya pia.

"Uwepo wa huduma za dharura utarahisisha utendaji kazi wa watumishi na kuongeza imani kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa katika hospitali yetu,"amesema Dkt.Jabir.

Pia ameeleza kuwa, uwepo wa huduma hizo za dharura zitasaidia kuokoa maisha ya watu kirahisi.

Jumla ya shilingi Bilioni 203 zimetumika katika ujenzi wa majengo haya muhimu kwenye utoaji wa huduma za afya nchini.

Post a Comment

0 Comments