Serikali yadhamiria kutokomeza VVU

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau na washirika mbalimbali wa kimataifa wanaounga mkono utoaji wa huduma za afya hususani katika Afua za Mapambano dhidi ya UKIMWI.
Hayo yamelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt.Festo J. Dugange (Mb) jijini Dar es salaam wakati akifunga mkutano wa kikanda uliohusisha nchi 11 za Afrika na nchi tatu kutoka Ulaya uliolenga kujadili namna ya kutumia rasilimali fedha katika afua za UKIMWI na kuboresha huduma za afya msingi.

Dkt.Dugange amesema,mkutano huo umewawezesha wataalam kujenga uwezo wa kufanya tafiti za gharama nafuu hasa kwa kutumia mbinu, kuendeleza mabingwa wa mabadiliko katika nchi zetu, kujenga mitandao na fursa za ushirikiano zaidi.

Dkt. Dugange ametoa wito wa Wizara na taasisi za kisekta kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata katika kikao hicho mahususi kwenye eneo la UKIMWI kuboresha maeneo mengine ya afya nchini.

Amesema, Serikali imeelekeza nguvu kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya afya nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba katika majengo ambayo yamekamilika pamoja na kuongeza watumishi wa fani mbalimbali za afya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dkt,Ntuli Kapologwe amesema, Mpango wa kimataifa na Serikali ya Tanzania ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 ugojwa wa UKIMWI uwe umetokomezwa.

Amesema, katika mkutano huo wamekubaliana kila nchi washirika kuhakikisha inaweka viashiria ambavyo vitawezesha kufanyiwa tathimi ya rasmilimani fedha inayoelekezwa katika mpango huo,kutengeneza jukwaa la wataalam la kupeana uzoefu na kufanya vikao vya tathmini kila mwaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news