Simba SC yampa kandarasi ya miaka mitatu mshambuliaji Mohamed Mussa

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji, Mohamed Mussa kutoka Malindi ya Zanzibar.
Mussa ambaye mbali na kucheza kama mshambuliaji pia anamudu kucheza kama kiungo wa nafasi zote za pembeni amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo ya jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu hiyo, miongoni mwa sifa ambazo zimewafanya kuvutiwa na kumsajili mchezaji huyo ni kipaji chake halisi cha mpira pamoja umri wake wa miaka 22, "tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwa siku za usoni,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, ingawa anatokea Visiwani Zanzibar hii haitakuwa mara ya kwanza kushiriki Ligi Kuu ya NBC amewahi kuzitumikia timu za Gwambina FC na Mbeya City.

Usajili wa Mussa unakuwa ni wa nne katika dirisha hili dogo baada ya Saido Ntibazonkiza, Hamed Ismael Sawadogo na Jean Baleke na rasmi wamefunga usajili kwa wakati huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news