Tanzania ipo salama-Waziri Dkt.Tax

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Jamhuru ya Muungano wa Tanzania imekutana na wadau wa maendeleo wakiwemo mabalozi na wakuu wa taasisi za Kimataifa huku ikiwahakikishia watanzania na wadau hao kuwa nchi ipo salama na hakuna matishio yoyote ya kiusalama.

Hayo yamesema leo Januari 30,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.Stergomena Tax wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na wadau hao.

Serikali imetoa kauli hiyo baada ya uwepo wa uvumi kuwa kuna matishio ya kiusalama na vurugu ndani ya nchi hali iliyopelekea Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM),kusitisha safari zake nchini.

“Wiki iliyopita kulikuwepo na uvumi kuwa kuna matishio ya vurugu ndani ya nchi yetu hadi Shirika la Ndege la KLM, kusitisha safari zake nchini, serikali ilianza kuzifanyia kazi na polisi walitoa taarifa pia Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Makame Mbarawa, alitoa taarifa kuwa anga letu ni salama.

“Kutokana hali hiyo tumewaita wadau wa maendeleo wakiwemo mabalozi na kuwahakikishia kuwa hali yetu ni salama kabisa hakuna tishio lolote la kiusalama tunawahakikishia Watanzania na Dunia kwa ujumla kuwa Tanzania ni salama na tuwashukuru wale wote hata uwepo wa taarifa hizo waliendelea kuja nchini,”amesema Waziri Dkt.Tax.

Pia amesema kuwa, katika kikao hicho na wadau hao wamekubaliana kuwa hali hiyo haitajitokeza tena na wataendelea kufanya kazi kwa kushirikiana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news