Vipipi vinavyodaiwa kutumiwa na wanawake sehemu za siri vyapigwa marufuku Zanzibar

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wakala wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba Zanzibar (ZFDA) imemzuia mfanyabiashara, Maryam Shaaban Laurent kutoendelea kufanya biashara ya kuuza bidhaa za Lump Sugar (Vipipi) vinavyodaiwa kutumiwa na wanawake kujiweka sehemu za siri ili kupata mvuto na kubana maumbile yao.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ZFDA imetoa tahadhari ya kutotumika kwa vipipi hivyo huku ikiendelea kufanya msako wa kuviondoa sokoni.

Mkuu wa Divisheni na Vipodozi wa mamlaka hiyo,Salim Hamad Kassim amesema, wanazichukua sampuli za bidhaa hiyo na kuzipeleka maabara ili kujiridhisha.

Pia amesema,sababu nyingine ya hatari iliyopo kwenye bidhaa hiyo ni kuwa haina lebo, haina ujazo wala mwisho wa muda wa matumizi na vilevile haijulikani imetoka sehemu gani.

Maryam Shaaban Laurent alipohojiwa ili kuelezea vipipi hivyo amesema, amekuwa akiviuza kwa njia ya mitandao ya kijamii.

“Wateja wote nilikuwa najihakikishia kuwa hiki kitu hakina madhara ni cha asili, ndicho kilichonitia moyo kufanya hiyo biashara na sitofanya tena hadi vikibainika havina madhara,”amesema.

Katika hatua nyingine leo Januari 20, 2023 Wakala wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba Zanzibar (ZFDA) imeteketeza tani nne za chakula ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu katika eneo la Unguja Ukuu jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news