Wakoratia kusafiri eneo la Schengen bila pasipoti,waanza kutumia sarafu ya Euro

NA DIRAMAKINI

JAMHURI ya Croatia imejiunga na kanda ya sarafu ya euro na Eneo la Schengen usiku wa Jumamosi wa manane, hivyo kuungana na mataifa 26 ambayo yana wanachama milioni 420 katika eneo kubwa zaidi la kusafiri bila pasipoti duniani.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya,Bi. Ursula von der Leyen akiwa ameambatana na Rais wa Jamhuri ya Croatia,Andrej Plenković walipowasili Zagreb kwenye hafla ya Croatia kujiunga na Eneo la Schengen na Eurozone, pamoja kutokana na usaidizi wa karibu wa halmashauri hiyo.Plenković alisema, hii ni hatua njema kwa wana Croatia na uchumi huku akisisitiza kuwa,malengo hayo ya kimkakati ni hatua kubwa na nzuri mbeleni. (Picha na Ikulu Croatia).

Kwa msingi huo, kuanzia Januari Mosi, 2023, Croatia ni mwanachama wa 27 wa eneo la Schengen, baada ya miaka 10 ya uangalizi chini ya uanachama wa Umoja wa Ulaya.

Taifa hilo lilijiunga na EU mwaka 2013, lakini ili kujiunga na eneo hilo ilibidi kutimiza masharti ambayo yalitajwa kuwa ni magumu ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuwa na kiwango himilivu cha ubadilishaji wa fedha, kudhibiti mfumuko wa bei na matumizi mazuri ya fedha za umma.

Aidha, tayari udhibiti wa mipaka kwenye mipaka ya nchi kavu na baharini na wanachama wengine wa EU umeondolewa, na ukaguzi kwenye mipaka ya anga utaondolewa kuanzia Machi 26.
Eneo la Schengen, ambalo limepanuka sasa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10,linajumuisha mataifa 23 kati ya 27 wanachama wa EU, pamoja na Iceland, Liechtenstein, Norway na Uswisi.

Norway, Iceland, Liechtenstein ni wanachama wa Eneo la Uchumi wa Ulaya (EEA), lakini si wanachama wa Umoja wa Ulaya huku Uswisi ikiwa ni mshirikia wa Eneo Uhuru la Biashara barani Ulaya (EFTA) na si mwanachama wa EU wala EEA.

Bulgaria na Romania si sehemu ya eneo la Schengen kwa vile uandikishaji wao haukupewa idhini na wanachama wengine mapema Desemba,mwaka jana wakati idhini ilipotolewa kwa Croatia. Pia Cyprus na Ireland hazipo katika eneo hili la usafiri bila pasipoti.

Eneo la Schengen linatajwa kuwa na urefu wa zaidi ya kilomita za mraba milioni nne, na hadi sasa lina wakazi wapatao milioni 420, kulingana na tovuti ya Baraza la Ulaya.

"Kila siku karibu watu milioni 3.5 huvuka mipaka ya ndani kwa kazi au kusoma au kutembelea familia na marafiki, na karibu watu milioni 1.7 wanaishi katika nchi moja ndani ya eneo la Schengen wakati wakifanya kazi katika nchini nyingine.
"Wana Europe hufanya wastani wa safari bilioni 1.25 ndani ya eneo la Schengen kila mwaka, ambayo pia inanufaisha sana sekta ya utalii na kitamaduni,"imeeleza tovuti hiyo

Katika njia yake ya kujiunga na eneo la Schengen, Croatia ilikutana na mapendekezo 281 katika maeneo manane ya Schengen ambayo ilipaswa kuyafanyia tathimini ya kina na kuchukua hatua.

Ni historia

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya na makamishna kadhaa mwishoni mwa wiki walikaribisha kujiunga kwa Croatia kwenye eneo la kusafiri bila pasipoti la Schengen na eneo la euro, Januari 1, 2023 huku wakitaja hatua hiyo kama mafanikio makubwa kwa Croatia na Umoja wa Ulaya.

Ni baada ya kukutana na viongozi wa Croatia na Slovenia katika kivuko cha mpaka cha Bregana baina ya nchi hizo mbili za Balkan, ambacho kiliwekwa wazi katika dakika za mwanzo za mwaka 2023 wakati eneo la usafiri huria la Schengen lilipanuliwa na kuijumuisha Croatia. Von der Leyen alisema ilikuwa siku ya kuandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu.
"Ninaikaribisha Croatia kwa moyo mkunjufu katika eneo la sarafu ya euro na katika eneo la kusafiri bila pasipoti la Schengen. Kuanzia Jumapili hii, raia wanaoendesha gari kwenda na kutoka Croatia wanaweza kuanza kusafiri bila udhibiti wa ndani wa mpaka,” Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen alisema.

"Haya ni mafanikio makubwa kwa Croatia,ni ishara ya kushikamana kwake na EU, na ishara ya mshikamano katika eneo la euro kwa ujumla. Huu ni wakati wa kujivunia kwa EU, Croatia na raia wake.
"Kizazi kijacho cha Wakroatia kitakulia katika eneo la Schengen. Watu wataweza kusafiri kwa uhuru, biashara haitaathiriwa na ukaguzi. Usafiri usio na vizuizi utaleta matokeo yanayoonekana kwa watu wanaoshi mpakani, wanaofanya kazi katika pande mbili za mpaka au kuwa na familia katika pande zote za mpaka. Jamii zitaungana pamoja tena,"alisema.

Makamu wa Rais wa Tume, Valdis Dombrovskis alisema kwamba, "hii ni hatua muhimu kwa Croatia kuashiria ushirikiano wake kamili wa Ulaya, na muhimu kwa umoja wetu wa Ulaya," alisema huku Makamu wa Rais, Margaritis Schinas aliongeza kuwa, "Hii ni hatua muhimu kwa Ulaya ya Croatia na wanastahili. Pongezi zangu za dhati kwa Wakroatia wote.”

Kamishna wa Uchumi Paolo Gentiloni alisema kwamba, "Mwaka Mpya huu utakuwa mwema kwa watu wa Croatia.
"Hii ni hatua ya kihistoria kwa Croatia na kwa Umoja wa Ulaya kwa ujumla. Labda ninaweza kukiri, hakuna nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya ilipita safari ya ajabu kama hii katika miongo mitatu iliyopita, kutoka katika vitisho vya vita katika miaka ya 1990, hadi uanachama wa EU mwaka 2013 na sasa tayari wanafurahia manufaa mawili yanayoonekana zaidi ya ushirikiano wa EU," Gentiloni alisema.

Kamishna wa Mambo ya Ndani, Ylva Johansson, alibainisha kuwa kila mwanachama mpya wa Schengen anaifanya EU kuwa na nguvu zaidi.

"Ninajivunia kazi ambayo Tume na Croatia wamefanya pamoja ili Wakroatia wanufaike na hatua hii ya kihistoria. Kwa hali hiyo, ninasalia kujitolea kibinafsi kwa Romania na Bulgaria kuwa wanachama katika siku za usoni,"alisema.

Aidha, Croatia kuanzia Januari Mosi, 2023 imekubali euro kama sarafu yake na inakuwa nchi ya 20 wanachama wa EU na raia milioni 347 wa EU ambao wanatumia sarafu ya pamoja ya EU. Tayari, euro imechukua nafasi ya Kuna kama sarafu ya Croatia.

Kuhusu Schengen

Eneo la Schengen, ambalo linachukuliwa kuwa mojawapo ya mafanikio makubwa zaidi ya EU, lilianza mwaka 1985 kati ya nchi tano wanachama ikiwemo Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji, Uholanzi na Luxembourg.
Uanzishwaji wa eneo hilo ulitokana na Mkataba na Makubaliano yaliyofikiwa Juni 14, 1985 katika Mji wa Schengen, Luxembourg na nchi wanachama hao watano wa Umoja wa Ulaya.(Mashirika)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news