Watumishi Kasulu waonesha vipaji vyao

NA RESPICE SWETU

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imeendelea kuwa miongoni mwa halmashauri chache nchini zinazowakutanisha watumishi wake kwa kufanya bonanza.
Hayo yamedhihirika wakati wa bonanza la michezo la watumishi wa halmashauri hiyo lililofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Ualimu Kasulu.

Wakizungumza wakati wa bonanza hilo, baadhi ya mashuhuda kutoka katika halmashauri jirani za Buhigwe na Kasulu Mji walisema kuwa watafurahi iwapo katika halmashauri zao kutakuwa na mabonanza hayo.

Akizungumzia hali hiyo kwa masharti ya kutolitaja jina lake, mwalimu mmoja anayefanya kazi katika halmashauri ya Mji wa Kasulu amesema, wamekuwa wakitamani mabonanza hayo lakini hayo lakini hawana uhakika kama yatafanyika.
Katika bonanza hilo, jumla ya michezo 21 ilishuhudiwa ikiwahusisha watumishi kutoka katika idara za afya, elimu msingi, elimu sekondari, utawala na makao makuu.

Bonanza hilo lililotanguliwa na mbio za kuzunguka uwanja zilizoongozwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, lilihitimishwa na chakula cha usiku kwa watumishi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza kabla ya kutoa zawadi kwa washindi wa michezo ya bonanza hilo, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Joseph Kashushura amewashukuru watumishi wote walioshiriki kwenye bonanza hilo na kuwataka kuwa kitu kimoja.
Michezo iliyohusika katika bonanza hilo ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha, kuvuta kamba na kufukuza kuku. Mingine ilikuwa ni kukimbia kwenye magunia, kuruka juu na kuonesha vipaji.

Kupitia bonanza hilo, Kashushura amewaahidi watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kuwa ataendelea kuzishughulikia kero mbalimbali zilizopo kwenye halmashauri hiyo.

"Tumeanza kuzifanyia kazi baadhi ya kero hizo mfano ni tatizo la usafiri na tunaendelea kushughulkia makazi ya watumishi na sasa tutakuwa tunafanya bonanza kila robo ili tupate muda zaidi wa kukutana,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news