Yanga SC haikamatiki, Polisi Tanzania FC yaburuza mkia

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2022/ 2023 kwa alama 53 baada ya mechi 20.

Ni kupitia ligi hiyo ambayo inaundwa na klabu na timu 16 kutoka Tanzania Bara ambapo imeonekana kuwa na mvuto mkubwa zaidi.

Januari 16, 2023 bao pekee la mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 64 liliipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa ligi hiyo.

Mtanange huo ulipigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Azam FC waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Ni kupitia mtanage uliopigwa katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Yona Amos aliyejifunga dakika ya tano, Abdul Suleiman (Sopu) na Kipre Junior dakika ya 70.

Mambo yalivyo

Mbali na Yanga kushikilia nafasi ya kwanza, nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo inashikiliwa na Simba SC ambayo ina alama 44 baada ya mechi 19.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na Azam FC baada kwa alama 43 baada ya mechi 20 huku nafasi ya nne ikishikiliwa na Singida Big Stars FC kwa alama 37 baada ya mechi 19 ambapo nafasi ya tano inashikiliwa na Geita Gold FC ambayo ina alama 27 baada ya mechi 20.

Wakati huo huo, Polisi Tanzania FC inaburuza mkia kwa alama 14 baada ya kucheza mechi 20 huku Ruvu Shooting FC ikifuata kwa alama 14 baada ya mechi 20.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news