Dkt.Mipawa Traders Company Limited yawakutanisha bodaboda



NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Dkt.Mipawa Traders Company Limited imewakutanisha madereva bodaboda na wadau wanaoweza kuwapatia mikataba ya mikopo ya gharama nafuu.Wadau hao ni Banki ya Equity pamoja na wasambazaji wa pikipiki aina ya Hero, Hunter.

Akizungumza hivi karibuni katika mkutano huo Mkurugenzi wa Dkt. Mipawa Traders Company Limited, Dkt. Salim Mipawa amesema kwamba amekuwa akiwasaidia vijana wa bodaboda kupata mikataba bora ya mikopo ya bodaboda.

“Tumekuwa tukitafuta wadau kwa ajili ya kuwapatia mikataba iliyo bora, leo tumewakutanisha na Equity Benki na Hero.

Hivyo lengo ni kutaka Bodaboda wajue biashara inayofanywa na Eauity Banki pamoja na Hero,” amesema Dkt. Mipawa.

Kwamba jambo hilo limelenga kumfanya dereva bodaboda amiliki chombo chake ndiyo maana wamewakutanisha na wasambazaji wa bodaboda na watoa mikopo.

“Lengo kuu ni kutaka wajikwamue kiuchumi,” ameongeza Dkt. Mipawa.
Kwa upande wake Meneja Mahusiano wa Equity Banki Emerda Kihenga amesema wametafuta njia rahisi ya kusaidia vijana kupata bodaboda na bajaji.

Kwamba ili kijana uweze kupatiwa mkopo kwa ajili ya bodaboda na bajaji ni lazima awe na akaunti ya benki hiyo.

Hivyo amesema baada ya kuwa na akaunti hiyo kwa anayehitaji bodaboda atatakiwa kuchangia sio chini ya shilingi 613,000 huku muda wa marejesho ikiwa ni miezi 12 ambapo kila mwezi ni shilingi 62,000 kwa wiki na shilingi 8,900 kwa siku.

Kwa anayehitaji mkopo wa bajaji Emerda amesema atatakiwa kuchangia sio chini ya shilingi milioni 1,780,000 kwa muda wa marejesho wa miezi 18.

“Merejesho ni shilingi 127,000 kwa wiki na shilingi 18,100 kwa siku. Muda wa marejesho wa ndani ya miezi 12, maresho kwa wiki ni shilingi 180,000 na 26,000 kwa siku,” amesema.

Kwa upande wake David Jonas ambaye ni dereva bodaboda ameshukuru mchango mkubwa wa Dkt. Mipawa katika mafanikio yake kwani hadi sasa anamiliki bodaboda tatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news