Mheshimiwa Mchengerwa ashiriki Baraza la Madiwani

NA JOHN MAPEPELE

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, MNEC wa Mkoa wa Pwani na Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka madiwani wa Rufiji kutanguliza mbele maslahi ya Wananchi wakati wote wa maamuzi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Mheshimiwa Mchengerwa ameyasema haya Februari 8, 2023 kwenye mkutano maalum wa Baraza la madiwani wa Rufiji kujadili Taarifa ya Ugawaji wa Ardhi ya Rufiji kwa wawekezaji waliojitokeza kuwekeza.

"Niwaombe sana tutangulize maslahi ya wananchi wa Rufiji kama miradi tunakwenda nao tunasema utatuwezesha kuwapatia ajira wananchi wetu zaidi ya elfu kumi hatuna sababu ya kumkataa mwekezaji," amefafanua Mhe. Mchengerwa wakati alipokuwa akizungumzia miradi wa uzalishaji wa sukari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news