MWENYEKITI MPYA BODI YA REA AANZA KAZI RASMI NA KUSISITIZA UCHAPAKAZI, UADILIFU

NA VERONICA SIMBA-REA

MWENYEKITI mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini, Janet Mbene ameanza kazi rasmi kwa kukutana na kuzungumza na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ambapo amesisitiza uchapakazi, weledi, uadilifu na ushirikiano katika kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy akieleza majukumu ya Wakala hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini, Janet Mbene (katikati) katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 11, 2023.

Katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 11, 2023 na kuhudhuriwa pia na Wajumbe wa Bodi, Mwenyekiti amehamasisha kufanya kazi kwa ufanisi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa katika kuwasaidia wananchi hususan wa vijijini kupata maendeleo.
Wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini, Janet Mbene (hayupo pichani) wakati wa kikao baina ya Mwenyekiti na Menejimenti hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 11, 2023.

“Tujitahidi sana kufanya kazi vizuri, kwa weledi na kwa wakati huku tukisimamia maeneo ambayo tunapaswa kuyasimamia kwa karibu sana hasa wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali,” amesisitiza Mwenyekiti.

Akizungumza zaidi, Mbene ameeleza kuwa maendeleo ya kiuchumi yanategemea sana nishati za aina zote, hivyo akatoa hamasa kwa wafanyakazi wa REA kupitia Menejimenti kutumia vizuri rasilimali kidogo zinazopatikana ili tija yake ionekane.
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini, Janet Mbene akizungumza na Wajumbe wa Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Februari 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

Amesema REA ni Taasisi yenye umuhimu mkubwa kwa Taifa kutokana na mchango wake katika maendeleo hususani ya wananchi wa vijijini. “Na kwa hali hiyo hii kazi tuliyopewa siyo ndogo,” amesisitiza.

Zaidi, Mwenyekiti amewataka wote kuhakikisha wanafanya kazi inayoacha alama na kwa namna hiyo kuzitendea haki nafasi walizopewa kuwatumikia Watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy akieleza majukumu ya Wakala hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini, Janet Mbene (katikati) katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 11, 2023.

Akizungumza kwa niaba ya Menejimenti na Wafanyakazi wote wa REA, Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Hassan Saidy amemhakikishia Mwenyekiti ushirikiano na kwamba watatekeleza yote aliyoyaagiza.

Awali, Wajumbe wa Menejimenti walipata fursa ya kujitambulisha kwa Mwenyekiti na kila mmoja kueleza majukumu yanayotekelezwa katika Idara/Kitengo anachosimamia.
Wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini, Janet Mbene (hayupo pichani) wakati wa kikao baina ya Mwenyekiti na Menejimenti hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 11, 2023.

Janet Mbene aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Februari Mosi, 2023 na kutangazwa Februari 3, mwaka huu kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini baada ya Mtangulizi wake kumaliza muda wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news