WAZIRI CHANA: SERIKALI IMEWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI SEKTA YA UTALII

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kutaka kuwekeza kwenye Sekta ya Utalii nchini ili kuweza kutafsiri kwa vitendo maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya The Royal Tour.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akikabidhiwa tuzo iliyotolewa na na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Usafiri wa Anga Tanzania (TASOTA) Moustafa Khataw ikiwa ni kutambua mchango wake katika wa kuhakikisha Wanachama wa TASOTA wanafanya kazi zao katika mazingira wezeshi ikiwemo kero zao kutatuliwa kwa wakati.

Ametoa kauli hiyo jana usiku jijini Dare s Salaam wakati akizungumza na Chama cha Mawakala wa Usafiri wa Anga Tanzania (TASOTA) kwenye mkutano wao wa mwaka ambapo kila mwaka hukutana mara moja kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusu ustawi wa chama chao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akiwa ameongozana Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA),Moustafa Khataw ( wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) ....Mfugale mara baada ya kuwasili kaatika mkutano wa mwaka wa TASOTA uliofanyika jana usiku.

Amesema Serikali imepunguza ada ya kila mwaka kwa Mawakala wa Usafiri wa anga nchini ( TALA fee ) kutoka dola za Marekani 2,000 hadi dola 500.

Pia ameeleza kuwa Serikali imejipanga kupunguza utitiri wa kodi katika sekta ya utalii ili kuhamasisha Wawekezaji zaidi katika sekta hiyo ili iweze kutoa ajira nyingi zaidi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA),Moustafa Khataw ( wa kwanza kulia ) wakiwa kwenye mkutano wao wa kila mwaka wakifuatilia burudani jana Jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuwekeza miundombinu bora katika maeneo ya Hifadhi ikiwemo barabara zenye uwezo wa kupitika muda wote pamoja na usimikaji wa mtandao wa intaneti katika mlima Kilimanjaro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akizungumza na Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA) kwenye mkutano wao wa mwaka ambapo amewapongeza kwa kuwa wazalendo wa kuilinda na kutetea nchi kwa watalii wanaoitembelea Tanzania.

Amesisitiza kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kuondoa vikwazo kwa wadau wenye nia ya kutaka kuwekeza hapa nchini.

Akizungumzia umahiri wa TASOTA, Waziri Chana amesema Wanachama hao wamekuwa wazalendo na Mabalozi wa kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa wageni wanaotaka kuja kujionea uzuri wa Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi wa Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA) katika mkutano wa mwaka wa Chama hicho uliofanyika jana usiku Jijini Dar es Salaam.

"Najisikia fahari kuona TASOTA, wakifanya kazi usiku na mchana ya kuilinda na kuitetea taswira ya nchi kwa kuratibu na kupanga safari za watalii wanaotembelea Tanzania."
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA) pamoja na wageni waalikwa wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana ambapo amekipogeza Chama hicho kwa kazi kubwa inayofanya ya kutangaza vivutio vya utalii kwa watalii wanaokuja kuangalia vivutio vyetu.

Aidha, Dkt.Chana ameihaikikishia TASOTA kuwa yeye kama Waziri mwenye dhmama ataendelea kufanya kazi kwa ukaribu na jumuiya hiyo ili sekta ya utalii iweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

Naye Mwenyekiti wa TASOTA, Moustafa Khataw amesema anaishukuru Serikali kwa kutambua mchango wao wa kutangaza uzuri wa Tanzania.
Mwenyekiti wa TASOTA, Moustafa Khataw akizungumza kabla hajamkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Dkt.Pindi Chana ambapo ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wao wa kutangaza uzuri wa Tanzania.

"Tumekuwa tukifanya kazi zetu kwa weledi wa hali ya juu katika tasnia hii ya usafirishaji kwani ni biashara hii haina njia za mkato wala haina ujanja ujanja inahitaji watu wazalendo na wenye haiba nzuri katika kuwahudumia watalii wetu," amesema Mwenyekiti Khataw.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news