Serikali yatoa mtambo wa kuchakata Hewa ya Oksijeni katika Halmashauri ya Tunduma

NA WILLIAM MAGANGA

SERIKALI imetoa kifaa cha kisasa cha kuzalisha hewa ya Oksijeni pamoja na mitungi 63 itakayomsaidia mgonjwa mwenye shida ya upumuaji sambamba na vifaa vya upasuaji na upimaji katika Halmashauri ya Mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe.
Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo, Dkt. Enock Mwambalaswa amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta vifaa hivyo na bado gharama yake haijatolewa, kwani bado vifaa vingine vinaendelea kuja na kwamba kinu hicho cha kuzalisha hewa kitaweza kuhudumia wagonjwa wa ndani na nje ya Tunduma.
Amesema ,sambamba na hilo pia Serikali imewapa vifaa vya shilingi milioni 370 vikiwemo vya upasuaji hali nitakayoongeza utoaji wa huduma za matibabu na kumudu wingi wa watu hasa ukichukulia Tunduma ni Lango Kuu la nchi za SADC, hali iliyopelekea kuwa na mwingiliano mkubwa wa watu.

Dkt.Mwambalaswa amesema, vifaa hivyo ni vya kisasa zaidi kama kifaa kinachoruhusu hewa ya Oxjeni kumfikia mgonjwa (Flow meter with humidifier), kifaa cha kupimia umeme kwenye moyo (Electro cardiograph), Kifaa cha kubebeka cha mionzi laini (portable ultrasound), Kifaa cha kupimia macho (wall mounted ophthalmoscopes), na Kifaa cha mionzi mizito (X-Ray ).
Alivitaja vifaa vingine kuwa ni Meza ya kubebea wagonjwa (stretchers), Mtambo wa kuchakata na kutunza hewa ya Oxjeni (PSA Oxygen generating plant),Vifaa anavyo vaa mtaalam kujikinga na mionzi (Protective gear for X-Ray), Vifaa vya kumuongezea mgonjwa hewa ya Oxjeni (ventilator) na vifaa mbalimbali vinavyosaidia wakati wa upumuaji (Endotracheal tubes).

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Philemon Magesa amesema, “Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa kupata matibabu salama kwa kuwapatia vifaa hivi, ni jukumu letu sasa wataalamu kuvitumia kwa weledi na uadilifu ili vidumu katika kuwatibu walengwa,”alisisitiza Mkurugenzi Magesa.
Aliongeza kuwa mbali na hilo, “Serikali imetupatia fedha zinazotumika kujenga vituo vitano vya afya lengo ni kuhakikisha wananchi wa Mji wa Tunduma wanasogezewa huduma karibu huku Halmashauri kwa kutumia fedha za mapato ya ndani asilimia 70 tunazitumia kujenga miradi ya maendeleo,” alisema Magesa

Tunduma ni lango kuu la nchi za SADC hivyo, kutokana na mwingiliano mkubwa wa wananchi wanaoutumia mpaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameona aongeze nguvu kwenye sekta ya afya kuongeza uhakika wa matibabu kwa wananchi wa ndani na nje ya Tunduma
Kwa upande wa wananchi wa Mji wa Tunduma akiwemo Isakwisa Mwashilindi alisema wana kila sababu ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuwajali wananchi wake kwa kuleta vifaa vya aina hiyo na kwamba huduma za afya zimeboreshwa mara dufu ukilinganisha na ilivyokuwa awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news