Simba tunafunga pamoja, tunafungwa pamoja-Mo Dewji

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Heshima na mwekazaji wa Klabu ya Simba, Bilionea Mohamed Dewji (Mo Dewji) amesema,mashabiki wa klabu hiyo hawapaswi kukata tamaa baada ya jana kupoteza nyumbani dhidi ya Raja Casablanca.

Mo amesema, wanatakiwa kuendelea kuwaunga mkono wachezaji wao na kuwapa sapoti sio kuwavunja moyo huku akisisitiza si mara zote utapata matokeo mazuri.

“Simba tunafunga pamoja, tunafungwa pamoja. Hatukati tamaa. Tutaendeleza mapambano,”amesema MoDewji.

Ikumbukwe kuwa, mchezo Februari 18, 2023 Simba SC ya jijini Dar es Salaam katika mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca kutoka Morocco uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ulimalizika kwa kupoteza mabao 3-0.

Simba SC walianza mchezo kwa kasi kutafuta bao la mapema, lakini Raja walikuwa makini huku wao wakifanya mashambulizi ya kujibu kila wanapopoteza mpira.

Hamza Khabba aliwapatia Raja bao la kwanza dakika ya 30 kwa shuti kali nje kidogo ya 18 baada ya kugongeana pasi kutoka katikati ya uwanja.

Kipindi cha pili, Simba SC ilirudi kwa kasi wakimiliki mpira zaidi, lakini Raja waliziba mianya yote huku wao wakiendelea kufanya mashambulizi ya kujibu.

Sofiane Benjdida aliwapatia Raja bao la pili dakika ya 83 baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Bentayg.

Dakika mbili baadae mlinzi wa kati wa Raja Ismail Mukadem aliwapatia bao la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi Joash Onyango kucheza madhambi ndani ya 18.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news