TASAF yastawisha ndoto za wanafunzi VETA mkoani Mara

NA MWANDISHI WETU

KAIMU Mkuu wa Chuo cha Ufundi VETA mkoani Mara, Mwalimu David Luis ameushukuru Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Tatu (TASAF) kwa jitihada inazozifanya kuwezasha vijana kupata ujuzi ambao utawasaidia kujiajiri au kuajiriwa ili waweze kuendesha maisha yao na familia pamoja na kujitoa kwenye janga la umaskini.
Mwanafunzi Asha Juma kutoka Mtaa wa Matare mjini Musoma ambaye anapata mafunzo ya ufundi bomba katika chuo hicho akiendelea na mafunzo kwa vitendo na mwenzake.
Elly Maduhu ambaye ni Mratibu wa TEA akitoa maelezo kwa maofisa kutoka TASAF Makao makuu pamoja na viongozi wa chuo hicho kuhusu mradi wa TASAF na TEA ambao umesaidia kufadhili wanafunzi mbalimbali kwa ajili ya kupata mafunzo katika chuo hicho.
Mwanafunzi Asha Juma kulia ambaye ni mnufaika na mradi wa TASAF pamoja na TEA pamoja na mwenzake wakiwa katika darasa la kompyuta wakiendelea na mafunzo ya kompyuta.

“TASAF walitulea vijana kumi na tatu ambao hapa chuoni wamegawanyika katika kozi tofauti ambapo katika fani ya kompyuta wapo vijana wanafunzi wanne, umeme wa majumbani wapo wanafunzi watano, fundi bomba yupo kijana mmoja, ufundi wa magari mwanafunzi mmoja, upande wa udereva pia kuna mwanafunzi mmoja,” amesema Mwalimu David.
Mwalimu David Luis ameyasema hayo wakati akizunguma na timu ya wataalam wa mawasiliano kutoka TASAF Makao Makuu waliotembelea katika chuo hicho ili kuona maendeleo ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho baada ya taasisi hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kuwapeleka wanafunzi 13 kutoka kaya masikini ili kupata ujuzi wa ufundi ili watakapomaliza masomo yao waweze kujiajiri au kupata ajira na kuendesha maisha yao.
Ameongeza kwamba TASAF waliwaletea kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 11 pesa ambazo wanufaika hao wanagharamiwa kwenye ada, nauli na chakula cha mchana wanapokuwa hapa chuoni kwa ajili ya mafunzo

Aidha, Mwalimu David amesema kwamba kuhusu changamoto ya mabweni katika chuo hicho tayari Serikali kupitia Bajeti ya fedha ya 2022/2023 ilishawapangia zaidi ya shilingi milioni 900 ambazo zimetegwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mabweni katika chuo hicho, lakini pia wana chuo kingine ambacho kipo katika hatua ya mwisho wilayani Butiama na tayari kina mabweni na kitakapokuwa tayari wataweza kupokea wanafunzi wengi zaidi.
Kwa upande wake Elly Maduhu ambaye ni mratibu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) mkoani Mara amesema kwamba, mwaka 2010 walibahatika kupata mradi wa TEA kupitia SDF walipewa kiasi cha shilingi milioni 80 ambazo waliweza kusajili wanafunzi 280 katika fani ya ufundi wa kompyuta na matumizi ya kompyuta, wanafunzi wote hao tayari wameshahitimu mafunzo yao na baadhi yao wameajiriwa na wengine wamejiajiri.

Ameongeza kwamba, kupitia TASAF waliweza pia kupata mradi kupitia kaya maskini ambapo wanafunzi kumi na tatu kati yao wanafunzi nane tayari wameanza mafunzo na wengine watawasili kwenye chuoni hapo muda si mrefu.
Muonekano wa Darasa la Kompyuta katika Chuo cha Veta mkoani Mara mjini Musoma.
Mwanafunzi Asha Juma kutoka Mtaa wa Matare mjini Musoma ambaye anapata mafunzo ya ufundi bomba katika chuo hicho akiishukuru TASAF kwa kumpatia nafasi ya kusoma katika chuo hicho ambapo ameahidi kutoichezea nafasi hiyona kusoma kwa bidii ilikujikwamua katika hali ngumu ya maisha na umasikini.

Mwanafunzi Asha Juma ambaye ni mnufaika na mradi wa TASAF pamoja na TEA ametumia nafasi hiyo kutoa shukurani zake kwani kupitia miradi hiyo ameweza kupata mafunzo ambayo yatamsaidia kuajiriwa au kujiajiri na kuendesha maisha yake ya baadae.

Naye Mabonera ambaye ni mwanafunzi wa ufundi Seremala katika chuo hicho ameishukuru TASAF na TEA kwa kumpatia ufadhili wa mafunzo ambapo amewashauri vijana wengine watakaopata nafasi kupitia miradi hiyo kuzitumia nafasi hizo kwa kujifunza kwa bidii kwa ajili ya manufaa yao ya baadae.Afisa kutoka Dawati la Malalamiko TASAF akizungumza na wanafunzi katika moja ya madarasa ya chuo hicho ambapo amewaasa kusoma kwa bidii ili waweze kupata ujuzi ambao utawasaidia katika maisha yao mara watakapoondoka chuoni hapo nakuingia mtaani.
Picha mbalimbali zikionesha wanafunzi wakiendelea na mafunzo kwa njia ya vitendo katika fani mbalimbali chuoni hapo.

Mwanafunzi Asha Juma kutoka Mtaa wa Matare mjini Musoma ambaye anapata mafunzo ya ufundi bomba katika chuo hicho kwa upande wake ameishukuru TASAF kwa kumpatia nafasi ya kusoma katika chuo hicho ambapo ameahidi kutoichezea nafasi hiyo na kusoma kwa bidii ili kujikwamua katika hali ngumu ya maisha na umasikini kwa maisha yake ya baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news