Uongozi wa Wizara ya Nishati Zambia watembelea mitambo ya kupokelea gesi asilia Kinyerezi inayomilikiwa na TPDC

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati nchini Zambia, Mhandisi Bi. Himba Cheelo amefanya ziara ya kikazi kutembelea mitambo ya kupokelea gesi asilia Kinyerezi inayomilikiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).
Mhandisi Cheelo amesema kuwa, lengo la ziara yake ni kujifunza namna Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la uzalishaji na usambazaji wa gesi asilia kwa matumizi mbalimbali kama vile uzalishaji wa umeme, viwandani, kwenye magari na majumbani.

Bi. Cheelo aliendelea kwa kusema kwamba, "Zambia imefanya mabadiliko makubwa katika suala zima la uagizaji na uingizaji wa mafuta ya Petroli ambapo kufikia Septemba 30,2022 Serikali ya Zambia ilijiondoa rasmi katika jukumu la kuagiza mafuta ya petroli na kuachia jukumu hilo wa sekta binafsi.

"Ziara yetu inalenga kujifunza namna ambavyo Tanzania imepiga hatua katika suala zima la gesi asilia pamoja na uagizaji wa mafuta ya Petroli," alisema Bi.Cheelo.
Mhandisi Cheelo alipokelewa na Mwenyeji wake ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Heri Mahimbali.
Aidha, Mhandisi Cheelo alipata fursa ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi inayomilikiwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO).

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Tanzania),Heri Mahimbali alisema, "tunafurahi kupokea ugeni huu na tupo tayari kuwapatia ushirikiano kwa ajili ya wao kujifunza namna ambavyo Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Rais Samia imepiga hatua katika eneo la nishati hasa gesi asilia, umeme pamoja na mafuta ya Petroli."

Mhandisi Cheelo ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, atatembelea pia kituo cha kujaza gesi asilia kwenye magari kilichopo Ubungo jijijni Dar es Salaam,Karakana ya DIT inayohusika na kubadili Mifumo ya magari kutumia GESI ASILIA, Taasisi ya Uagizaji wa Mafuta (PBPA), Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Nishati na Maji-EWURA pamoja na kampuni Tanzu ya kuzalisha nguzo za umeme za Zege inayomilikiwa na TANESCO.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news