Waaswa kutenga muda wa kusikiliza changamoto za wananchi

NA MWANDISHI WETU

MLEZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa,Bi.Leila Ngozi ametoa rai kwa viongozi wa serikali kuendelea kutenga muda kwa ajili kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Bi.Leila Ngozi akihutubia katika maadhimisho ya miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi katika Kata ya Ipera Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma.

Wito huo umetolewa Februrai 5, 2023 wakati wa kumbukumbu ya miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi iliyofanyika katika Kata ya Ipera Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma.

Leila ameomba viongozi kuendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo wana CCM wanajivunia imefanya mambo mengi.
Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Bi.Leila Ngozi alipomtembelea Mjumbe wa Shina namba Moja wa Chama Cha Mapinduzi.

Ameongeza kuwa, Ilani imeelekeza katika sura ya 10 ibara ya 251, “kuwa tunatakiwa tutenge muda wa kwenda kusikiliza wananchi wetu, Niwaombe wananchi tuendelee kueleza changamoto zetu kwa viongozi wetu ili waweze kuzifanyia kazi,”amesema Leila.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa ametoa rai kwa watendaji wa Serikali kutenda haki katika maamuzi na kuepuka dhuluma na uonevu.

“Wanachi toeni taarifa kama kuna mienendo isiyofaa kwa watendaji wa Serikali katika kutoa huduma,” amesema Alhaj Kimbisa.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule amesema, ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezeka kwa kasi kubwa kutokana na dhamira ya dhati ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa ambaye pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

“Upo mradi mkubwa wa umwagiliaji ambao upo katika hatua nzuri ya ujenzi, na mradi wa ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa ambao umeshakamilika na Mheshimiwa Rais ameridhia ujenzi wa barabara ya lami ili kuunganisha barabara Wilaya ya Mpwapwa kwa lami,”amesema Mkuu wa Mkoa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akiteteta neno na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene amesema furaha ya watu wa Ipera ni kukamilika wa Kituo cha afya cha Ipera.

“Tunajivunia maendeleo, lakini lazima tuendele kufanya kazi na tujitegemee katika kujenga taifa,” alisema Waziri Simbachawene.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news