Waziri Dkt.Mabula ateta na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORECORP Limited ya Australia

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM 

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORECORP Limited ya nchini Australia, Bw. Henk Diederichs.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula (kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORECORP Limited ya Australia, Henk Diederichs jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari 2023. Kampuni ya ORECORP Limited imeingia ubia na Kampuni ya Sotta Mining Limited yenye ubia na Serikali kuchimba dhahabu eneo la vijiji vya Sotta na Nyabila vilivyopo Igalula Sengerema mkoani Mwanza.  

Mazungumzo baina ya Waziri Dkt.Mabula na Mtendaji Mkuu huyo wa ORECORP Limited yamefanyika jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Dkt. Allan Kijazi na Mthamini Mkuu wa Serikali, Evelyne Mugasha.

Kampuni ya ORECORP Limited imeingia ubia na kampuni ya Sotta Mining Limited yenye ubia na serikali na kuunda kampuni ya uchimbaji madini ya Nyanzaga Mining Corporation Limited ambapo Sotta Mining Corporation inamiliki asilimia 84 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki asilimia 16.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sotta Mining Corporation Limited-Africa, Damien Valente akizungumza wakati wa kikao baina ya uongozi wa ORECORP Limited na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari 2023.

Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Nyanzaga inatarajia kuchimba dhahabu eneo lenye ukubwa wa 23.36 kilometa za mraba lilipo vijiji vya Sotta na Nyabila kata ya Igalula wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa ajili ya shughuli za uchimbaji na ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayotumiwa na mgodi huo ambapo ili kampuni hiyo kuanza shughuli zake inatakiwa kutwaa ardhi kwa mujibu wa sheria kwa kuhakikisha wananchi wanalipwa fidia stahiki na kupisha katika eneo hilo.
Mthamini Mkuu wa Serikali, Evelyne Mugasha akizungumza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORECORP Limited- Australia, Bw. Henk Diederichs (kushoto) na Meneja Mkuu Sotta Mining Corporation - Afrika, Bw. Damien Valente (katikati) wakati Waziri wa Ardhi, Dkt.Angeline Mabula alipokutana na uongozi wa ORECORP Limited tarehe 14 Februari 2023.

Kampuni ya uchimbaji dhahabu Nyanzaga ilitoa kandarasi kwa kampuni ya Uthamini ya Ace Consultants LTD ya kutekeleza zoezi la uthamini wa mali za wananchi wanaotakiwa kupisha shughuli za uchimbaji.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt.Angeline Mabula (wa tatu kulia) akiwa katika picha na ujumbe wa kampuni ya uchimbaji madini ya Nyanzaga pamoja na Wizara ya Ardhi walipokutana jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari 2023. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news