Waziri wanne Utamaduni mwanamke

NA ADELADIUS MAKWEGA

“Wakoloni walifanya kila wawezalo kudumaza sekta za Utamdauni, Sanaa na Michezo ambapo vijana wake waliokuwa mstari wa mbele kudai uhuru walihakikisa hawaendelezwi na kuwanyima elimu huku utamaduni wetu ulikashafiwa kuwa ni wa kishenzi na michezo haikupewa msukomo wowote.”

Balozi.Dkt.Pindi Chana.

Hayo yalikuwa maelezo ya Katibu Mkuu ndugu Sethi Kamuhanda aliyekuwa akisimamia wizara yenye sekta hizo mwaka 2011 wakati wa miaka 50 wa Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika.

Februari 15, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango wakati wa uapisho wa Waziri Dkt Pindi Chana kutumikia wizara hiii, Makamu wa Rais amesema kuwa sekta ya utamaduni inakuwa kwa kasi huku takwimu zake zinaonesha kuwa sasa inaajiri vijana wengi nchini Tanzania.

Hii inatoa picha namna serikali za awamu zote tangu uhuru zilivyojitahidi kufanya kazi ya kuibadilisha dhana potofu za wakoloni. Kazi hiyo imefanywa na wananchi wenyewe na viongozi wao katika ngazi mbalimbali tangu uhuru huo.

Siku ya leo mwanakwetu anajaribu kukupitisha katika majina yaliyoiongoza wizara hii kwa ngazi ya waziri uhuru hadi uteuzi wa Februari 14, 2023 uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Msomaji wangu isikupe tabu jina la wizara hiyo kubadilika badilika na baadhi ya sekta kubadilishwa, lakini mwaka 1962 wizara hii ilikuwa inatambulika kama Wizara ya Vijana na Utamaduni wa Taifa.

Mawaziri wake waliongoza ni kama ifutavyo;

Mhe.Oscar Kambona, wakafuata hawa, Mhe. Rashid Kawawa, Mhe. Idrisa Abdul Wakil, Mhe. Hashim Makame, Mhe. Jacob Namfua, Mhe Daud Mwakawago, Mhe Isaac Sepetu,, Mhe. Benjamin Mkapa, Mhe .Anne Makinda, Mhe. Ahmed Hassan Diria, Mhe. Dkt William Shija, Mhe. Philip Marmo, Mhe. Bakari Mbonde, Mhe. Dkt. Mohammed Seif Khatib, Mhe. Kingunge Ngombare Mwiru, Mhe. Edward Moringe Sokoine, Mhe. Michael Kamaliza, Mhe. Paul Bomani, Mhe. Joseph Rwegasira, Mhe. Paul Kimiti, Mhe. Sebastian Kinyondo, Mhe. Prof. Juma Kapuya, Mhe. Lawi Sijaona, Mhe. Sheikh Kaluta Amri Abeid, Mhe. Erasto Mang’enya, Mhe. Chediel Mgonja, Mhe. Jen. Mirisho Sarakikya, Mhe. Fatma Said Ali, Mhe. Charles Kabeho.

Mawaziri wengine walikuwa hawa ; Mhe. Prof. Philemon Sarungi, Mhe. Joseph J. Mungai, Mhe. Omar R. Mapuri, Mhe. George H. Mkuchika, Mhe Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara ,Mhe. Nape Nnauye, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Mhe. Innocent Bashungwa, Mhe. Omary Mchengerwa. Kwa sasa ni Mhe. Balozi .Dkt. Pindi Chana.

Mhe .Balozi. Dkt. Chana kwa hesabu ya orodha hiyo ni waziri wa 40 tangu Uhuru na waziri wanne mwanamke aliyewahi kuiongoza wizara hii.

Mawaziri arobaini na mawaziri wanawake wanne tu, Wanawake hao ni Mhe. Anne Makinda, Mhe. Fatma Said Ali, Mhe. Fenella Mukangara na sasa Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana.

Mwanakwetu upo?
Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com
0717649257

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news