Bandari kavu ya Kwala mambo tayari

NA MWANDISHI WETU

MENEJA Miliki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Alexander Ndibalema amesema,Bandari kavu ya Kwala iliyopo mkoani Pwani inatarajiwa kuanza kufanya kazi muda wowote.

Sambamba na kutoa huduma zote za kiforodha kama zinavyotolewa katika bandari zingine, kwani hatua zote za ukamilishaji wa bandari hiyo zimekamilika.

Ndibalema ameyabainisha hayo wakati akizungumzia kuhusiana na maendeleo ya bandari hiyo ambapo amesema ipo tayari kufanya kazi.

"Kwa sababu miundombinu yote ya msingi imekamilika na leseni zingine kutoka mamlaka zingine za Serikali zimeshakamilika,kinachosubiriwa kwa sasa ni kupata leseni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),”amebainisha.

Pia amesema, lengo kuu la kuanzishwa kwa bandari hiyo ni kuongeza ufanisi na kiasi cha shehena inayohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hatua ambayo itapunguza msongamano katika bandari hiyo pamoja na kuongeza mapato ya Serikali kupitia huduma zitolewazo katika bandari.

Meneja huyo amesema,bandari hiyo ina uwezo wa kuhudumia wastani wa makasha 823 kwa siku sawa na makasha 300,395 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 30 ya makasha yote yanayohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news