CR HOPE Foundation yaanza kuchunguzwa Zanzibar

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema kuwa, imepokea taarifa kuhusu Taasisi ya CR HOPE Foundation ambayo inasimamia skuli ndani ya Zanzimbar ambazo zinadaiwa kufundisha masomo yanayokwenda kinyume na maadili ya Mtanzania.

Hayo yameelezwa kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Hassan Kh.Hassan ikielezea kuhusu taasisi hiyo.

"Kumekuwa na taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa skuli ambazo zinafadhiliwa na Taasisi ya CR Hope Foudation zinazotumiwa kufundisha masomo ambayo ni kinyume na maadili ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

"Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepokea taarifa hii kwa uzito mkubwa na tayari imeshaanza kuifuatilia kwa umakini wa hali ya juu,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa sasa inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali katika kupata taarifa za uhakika kuhusiana na jambo hilo. "Na mara tu uchunguzi utakapokamilika wizara itatoa taarifa rasmi juu ya kadhia hii.

"Katika kipindi hichi cha uchunguzi wizara inatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuwa watulivu na kutoa mashirikiano ya karibu katika kufanikisha kupatikana kwa taarifa juu ya kadhia hii ili Serikali iweze kuchukua hatua stahiki baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo,"amefafanua Mkurugenzi huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news