Hiki hapa kikosi cha Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar leo

NA MWANDISHI WETU

KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam imetaja kikosi ambacho saa 10 jioni leo kitashuka katika Uwanja wa Manungu Complex kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja kulinganisha na kikosi kilichoanza mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Vipers.

Robertinho amemuanzisha mshambuliaji Jean Baleke akichukua nafasi ya Pape Sakho ambaye yupo benchi.

Kikosi kamili kilichopangwa:

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Jean Baleke (4), Moses Phiri (25), Saido Ntibazonkiza (39).

Wachezaji wa Akiba:

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Pape Sakho (10), John Bocco (22), Habibu Kyombo (32), Mohamed Mussa (14), Peter Banda (11).

Post a Comment

0 Comments