Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) yazindua programu ya kuwezesha wajane

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) linalojishughulisha na mapambano ya ukatili wa kijinsia Mkoa wa Mara chini ya Mkurugenzi wake, Rhobi Samwelly limezindua Programu ya Kuwawezesha Wajane kwa kuwajengea uwezo katika masuala ya kiuchumi, kiroho, kisheria na kuwaunganisha pamoja inayotambulika kwa jina la 'Erasto Widows Empowerment Programme.'
Uzinduzi wa programu hiyo umefanyika Machi 6, 2023 katika Kituo cha Nyumba Salama Kiabakari wilayani Butiama mkoani Mara na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali akiwemo Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Butiama, Atula Sanga,viongozi wa dini pamoja na kikundi cha Wajane cha Mwibagi kilichopo wilayani Butiama. 

Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania, Rhobi Samwelly amesema, programu hiyo inalenga kuwajenga wajane kiakili, kiroho na kisaikolojia katika kuhakikisha wanashiriki katika mambo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yao na Jamii kwa ujumla. 
Rhobi ameongeza kuwa, kupitia Programu hiyo Wajane wataweza kuunganishwa Kupitia vikundi katika kata hadi kuunda mtandao wa Wajane wa Mkoa wa Mara hadi Tanzania nzima.Ambapo wataweza kupewa mafunzo ya ujasiriamali, kufundishwa haki zao kisheria, kujitambua sambamba na kuwawezesha kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kuwapatia mitaji kupitia vikundi vyao. Na kuwajengea uwezo juu ya madhara ya ukatili wa Kijinsia na maswala yote mtambuka na maendeleo yao. 
Kwa upande wao baadhi ya wajane waliohudhuria uzinduzi wa programu hiyo wamempongeza Mkurugenzi wa Hope for Girls and Women in Tanzania, Rhobi Samwelly kwa maono hayo ambapo wamesema wataweza kunufaika na programu hiyo hasa kiuchumi, kiroho na kuweza kuwa na umoja utakowezesha mafanikio yao na jamii nzima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news