Huyu hapa Abdulhakeem Marunda (ABMA) Mtanzania anayefanya maajabu ya Muziki nchini Canada

NA ZAINAB KHAMIS

JAMHURI  ya Muungano wa Tanzania, ni nchi yenye baraka ya watu wenye vipaji vinavyotingisha kitaifa na kimataifa.

Utajiri huu wa Tanzania kubarikiwa kuwa taifa lenye vipaji lukuki katika fani na tasnia mbalimbali zinapambwa na kilemba au mbeleko ya lugha ya Kiswahili, ambayo ni lugha ya mwanzo ya kiafrika kutambulika kimataifa hadi kupewa siku maalumu na UNESCO kuwa kila ifikapo terehe 7 Julai ni siku ya kusherekea Kiswahili Duniani na hapa ndipo tunapomwangazia.
Abdulhakeem Marunda maarufu kwa jina la ABMA, Mtanzania anayefanya Maajabu ya Muziki nchini Canada. Muziki ambao unaoyeyusha barafu na kuleta joto kwenye msimu wa baridi kule nchini Canada.

Leo darubini yetu imeangazia nchini Canada na kugundua kuwa kumbe mwanamuziki
ABMA au Abdulhakeem Marunda ni mtanzania tena kutokea Mtwara.

Mwanamuziki mkazi nchini Canada, Mtanzania, mwenye asili ya Kusini mwa Tanzania, "Abma" jina lake la kuzaliwa ni Abdulhakeem Marunda aliyezaliwa Juni 20 mwishoni mwa miaka ya 70, katika moja ya Jiji kuu la Tanzania, Dar es Salaam, familia ilihamia kwenye moja ya miji mdogo huko Mtwara.

Ni Kusini mwa Tanzania ambako alikulia na kupata Elimu yake ya Msingi katika Shule ya Msingi Ligula (Mtwara) na baadae kuendelea na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Al- Muntazir Islamic Seminary iliyoko Upanga, jijini Dar es Salaam na kisha kwenda kumalizia Shule ya Sekondari Utete wilayani Rufiji  mkoani Pwani.

Alijaribu kujiunga na elimu ya juu ya sekondari, lakini hakuweza kumaliza, hivyo alirudi mtaani na kufungua darasa la kufundisha Kiingereza bure ili kuisaidia jamii yake iweze kupata urahisi wa kuwasiliana na wageni kutoka mataifa mengine.

Mapenzi yake katika Muziki yalionekana tangu alipokuwa mdogo, alitambulishwa katika ulimwengu wa Muziki akiwa na umri wa miaka saba na mjomba wake Bashir a.k.a "Sound" (ambaye wakati huo alikuwa ni DJ wa Muziki wa Mtaa) kutoka "Njinjo Disco Sound" kati ya miaka ya 80 hadi katikati ya 90's. Mapenzi yake katika Muziki yalipanda hadi pale ambapo alishindwa kujizuia, jambo ambalo lilimfanya aanze Kupenda Muziki wa Rap/Hip-Hop chini ya ushawishi wa Wasanii wengi wa muziki huo Rap/Hip Hop kama vile MC Hammer, Vanilla Ice, na baadaye kufuatiwa na Saleh Jabir, Mr. II a.k.a Sugu, Professor Jay na HBC, Nas,
B.I.G, 2Pac, Dr. Dre, Scarface, Jay-Z na wengine wengi, kama ilivyokuwa kwa vijana wengi katika umri wake.

Akiwa na umri wa miaka 17 alifanikiwa kuanza kuandika mashairi yake binafsi na alionekana kwa mara ya kwanza katika jukwaa mwishoni mwa mwaka 2001 baada ya Dj Rough NG' kutambua uwezo alionao “Abma” na kuamua kumpa nafasi ya kuonyesha kipaji chake ndipo alipewa nafasi ya kutumbuiza kama msanii mfunguzi kwenye shoo ya moja ya Mwanamuziki Mkubwa wa Hip Hop nchini Tanzania "Fid Q akiwa ameambatana na mwanamuziki Ragga “Hard Mard”.

Ni kwenye ziara iliyoandaliwa na kampuni ya Jojo'z Entertainment iliyokuwa ikiendeshwa na Jackson Namajojo (Mwanzilishi) na Abdillah Mbelenje, Mwaka 2005 “abma” Alifanikiwa kutoa wimbo wake wa kwanza uliokwenda kwa jina la "Nini Thamani..?" Iliyotayarishwa na Mandugu Digital Studio chini ya Usimamizi wa Mtayarishaji Shakii, kwa vile ulikuwa wimbo wenye utata wa kisiasa (Controversial) , wimbo huo haukupata kuchezwa katika  vituo vingi  vya redio nchini Tanzania.

Ilipofika mwaka 2012 alifanikiwa kutoa nyimbo yake ya pili iliyokwenda kwa jina la "They Keep Talkin' (Bado Wanaongea) akimshirikisha mwanamuziki “Otuck William" iliyotayarishwa chini ya mtayarishaji Geof Master katika studio za Waiz Records na KP Production mjini Mtwara akitumia jina lake la zamani la kisanii "A-Thug 79" ingawa nyimbo hiyo haikufanya vizuri lakini angalau ilimsaidia kuweka alama kwenye jukwaa la YouTube kwa Video iliyofanywa Waelekezaji wa Video (Video Directors) “Kikulacho Rashid” a.k.a “Kiku Bang” na “Dadi Namtema” wa “All 4 One Pictures” iliyokuwa inamilikiwa na rafiki yake “Kikulacho Rashid” a.k.a “Kiku Bang” na hivyo kumpa motisha kuwa anauwezo wa Kufanya anachokifanya na kutimiza ndoto.

Mnamo Januari 10, 2023 "abma" alifanikiwa kutoa Albamu yake ya kwanza inayoitwa "Installation" kwa Kiswahili “Usanikishaji”, “Abma” Anasema Maombi na Muziki ndio Tiba bora katika Maisha yake, iwe katika hali ya Juu au ya Chini, Anaposikiliza Muziki huweza kusikia na kutambua kila Ala iliyoko katika Muziki huo, kwake "Muziki Mzuri" ni "Muziki Mzuri tu".

Na Kauli Mbiu yake ni : Upendo kwa Wote, Bila chuki kwa Yeyote (Love for all, Hatred for none), na Tiba za Msongo kwake ni Sala, kisha Muziki (The Therapy for emotions to him is Prayers and then Music).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news