Kuiona Simba dhidi ya Horoya ni 3000/-

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam imesema, kiingilio cha chini katika mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya kutoka Guinea utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi kitakuwa shilingi 3000. 

Simba SC imebainisha kuwa, viingilio hivyo havina tofauti yoyote ya vile vya mchezo uliopita dhidi ya Vipers, kwa kuwa lengo ni kuhakikisha mashabiki wanavyojitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu.


Viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh. 3000 

VIP C Sh. 10,000

VIP B Sh. 20,000

VIP A Sh. 30,000

Platinum Sh. 150,000

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema tiketi za Executive nazo zitapatikana kwa ajili ya vikundi au makampuni ambayo yatataka kuwanunulia wafanyakazi wake watapelekewa mpaka ofisini kwao.

Aidha, tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao, mashabiki wanasisitizwa kununua mapema ili kuepeuka usumbufu siku ya mchezo.

"Mchezo wa Jumamosi ni kama fainali kwetu, tunahitaji ushindi ili kufuzu hatua ya robo fainali hivyo tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kuendeleza moto,"ameeleza.

Post a Comment

0 Comments