TANZIA:Kigogo wa CHADEMA afariki

NA DIRAMAKINI

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya chama hicho, Mzee Slyvester Kanyasi Masinde amefariki.

"Tunasikitika kutangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Mzee Slyvester Kanyasi Masinde kilichotokea alfajiri ya leo Machi 15, 2023 saa 11:25 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza alikokuwa amelazwa. Pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa chama;

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyololewa leo Machi 15, 2025 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema.

"Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, wajumbe wa bodi ya udhamini, marafiki, viongozi na wanachama wote wa CHADEMA kwa msiba huu mzito, Tutatoa taarifa za kina baada ya kikao na familia. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana na libarikiwe,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Novemba 19, 2021 mzee Silivester Kanyasi Masinde alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Arcado Ntagazwa ambaye alikuwa mwenyekiti.

Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inaundwa kwa mujibu wa Katiba ibara ya 8.3 toleo la mwaka 2019.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news