Mambo muhimu kwa maisha yako

NA BETHANIA SIMON

KUNA maeneo manne ya maisha yako ambayo unapaswa kuyapa kupaumbele sana ili uweze kufanya mambo makubwa katika maisha yako ya kuishi hapa duniani.

Picha na blog.rsrit

Maeneo yote haya manne ni muhimu na unapaswa kuyalinda kwa kuyafanyia kazi, kwa ajili ya ubora wa maisha yako mwenyewe unayoishi hapa duniani.

Maeneo hayo ni kama yafuatavyo;

1:Akili yako

Unapaswa kujijengea mtazamo sahihi wa kiakili ili uweze kufanikiwa. Mtazamo chanya na wa uwezekano utakaokusukuma kufanya makubwa Duniani,mtazamo ni muhimu sana kabla ya imani na elimu.

2.Afya ya mwili wako

Unapaswa kuwa na afya bora ya mwili ili uweze kufanikiwa. Itakuwa vigumu kupambania mafanikio yako ukiwa unaumwa umevunjika au umepooza au ukiwa umekufa,ndoto zako Duniani zitakua zimepote.

3: Hisia zako/jinsi ya kufikiria

Unapaswa kujenga hisia chanya zinazokupa msukumo wa kufanya zaidi ili kufanikiwa. Hisia chanya za upendo, matumaini na furaha ni muhimu kujiwazia vizuri na kuwawazia vizuri wenzako kwa mafanikio yako na uhusiano mzuri itakusaidia sana hii.

Hisia hasi za hofu, hasira, wivu na chuki kuwawazia wenzako vibaya unapaswa kukabiliana nazo kwa namna nzuri zaidi ili zisikuangushe au kukurudisha nyuma katika kukufedhehesha maishani.

4:Imani yako

Unapaswa kujijenga na kujiimarisha kiimani ili uweze kupambana kufanikiwa kwa kuvuka magumu na changamoto mbalimbali unazozipitia.

Imani ndiyo inakuwezesha kujitambua na kujisikiliza kisha kuweza kutumia uwezo mkubwa na wa kipekee uliomo ndani yako wewe mwenyewe kufanya maajabu.

Imani juu ya Mungu au juu ya chochote unacho kitaka kitokee imani ni muhimu mno kwako. Imani ndiyo huzaa matokeo yanayo onekana kwa macho ya damu na nyama. Linda pigania sanaiImani yako, sirudii. (Soma; Yuda 1:3).

Afya ya mwili wako

Kuna maeneo matatu muhimu ya kuzingatia ili kuwa na afya bora ya mwili wako huo:-

A.Eneo la kwanza ni mazoezi

Unapaswa kufanya mazoezi kila siku ili kuimarisha afya ya mwili wako. Mazoezi yanazalisha kemikali zinazoupa mwili nguvu na msukumo wa kupambana zaidi na hali hali za hii Dunia.

Pia mazoezi yanaimarisha kinga ya mwili na mtu kuweza kuepuka magonjwa mbalimbali yanayo wapata binadamu hata kama tumeokoka na unaomba kama baba yako jiwe la Mungu bado wewe upo ndani ya vazi la huo mwili unaoharibika.

Kuna mazoezi ya aina nyingi, lakini makubwa ni ya kukimbia na kunyanyua vitu vizito. Hayo yanauweka mwili wako katika afya nzuri kabisa kukimbia hulipii usije ukasema ooh mimi sina pesa nk.

B.Eneo la pili ni ulaji na unywaji

Unapaswa kula kwa usahihi ili uweze kuwa na afya bora kwa ajili ya mafanikio yako mwenyewe.
 
Eneo la ulaji kuna vitu vitatu;

Mosi,aina ya vyakula unavyokula, vinapaswa kuwa vyakula halisi na siyo vya viwandani. Kula zaidi mbogamboga na epuka wanga na sukari kwa wiki haya nimeyakopa kwa wataalamu kabisa.

Pili,kunywa maji mengi kwa kila siku, yanauweka mwili kwenye hali nzuri, isipungue lita tatu.

Tatu, kufunga, kuchagua siku ambazo huli au unakaa muda mrefu bila kula kunaufanya mwili wako ujifanyie matengenezo, lakini pia kunakuimarisha kiroho,katika hili mimi Bethania Simon sipo vibaya.

Eneo la tatu ni mapumziko

Mwili wako unahitaji mapumziko ya kutosha ili uweze kuwa na ufanisi na kubwa zaidi katika shughuli zako za kila siku.

Huwezi kufanikiwa kwa kufanya kazi usiku na mchana bila kupumzika, kumbuka wewe ni binadamu mwenye mwili ambao huchoka, kuchoka ni ubongo unatoa taarifa kwenye mwili kua pumzisha mwili sasa, ukilazimisha nakumwambia utafariki haraka maisha haya hayataki u-seriously ulio pitiliza, utaviacha vyote unavyotaabikia.

Kule Mbezi Beach Makonde kuna na Nabii alikua akijisifia katika saa 24 yeye analala saa 2 tu akadhania ni sifa, kifupi alikufa haraka wakamsingizia Mungu eti kampaisha hajafa.

Mwili ukishachoka huwezi tena kufanya shughuli zako kwa ufanisi mzuri.Hivyo unapaswa kupumzika ili mwili wako ujenge nguvu mpya na kujiponya pia.

Unapaswa kutenga muda wa kutosha wa kulala kulingana na mahitaji ya mwili wako. Unapokuwa umechoka.

Na pia unapaswa kuwa na mapumziko ya aina nyingine kwenye siku yako, kama kutembea,kusoma kitabu, kufanya mazungumzo na wengine.

Kufanya kazi kwa muda mrefu bila mapumziko ni chanzo cha uchovu ambao huwa kikwazo kwa mtu kufika kwenye mafanikio makubwa ya maisha yake.Tenga muda wa kupumzika na uheshimu ili uweze kufanya makubwa.Natumai kuna kitu umejifunza,mpenzi msomaji wangu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news