Mheshimiwa Chilo awafunda vijana

NA DIRAMAKINI

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Chilo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Uzini amewataka vijana kuzitumia maskani kujifunza vitu mbalimbali vitakavyowasaidia kuongeza kipato chao cha kila siku na kuacha kuwa tegemezi.

Kauli hiyo ameitoa huko Mpapa Wilaya ya Kat jijini Zanzibari wakati wa kukabidhi tv kwa vijana wa Maskani ya Bekari iliyopo Mpapa, amesema umefikia wakati kwa vijana kuzitumia maskani kuboresha hali zao za kiuchumi.

Aidha, amewaonya vijana hao kuacha kuonesha michezo itakayohamasisha vijana kujiingiza katika vitendo viovu ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kulevya, ujambazi na matendo mengine yasiofaa.

"Niwaambie ndugu zangu leo tumewapa television si kwamba itatuburudisha na kutufunza tu bali pia yaweza kuwa chanzo kwa vijana kuharibika kwa kuiga yasiofaa," alisema Naibu Waziri Chilo.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, Haji Shaaban Waziri amewaasa vijana hao kukemea na kutoa elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa lengo la kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuondosha vitendo hivyo.

Amesema, kwa sasa Zanzibar inakabiliwa na Janga la udhalilishaji huku takwimu zikionesha asilimia kubwa ya wafanyaji wa vitendo hivyo ni vijana.

Pia amewataka vijana kudai risiti za kielektroniki kila wanunuapo bidhaa ili kuzuia upotevu wa mapato ya Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news