Misaada ya kibinadamu iliyotolewa na Tanzania kwa waathirika wa kimbunga Freddy yavuka mpaka kuelekea Malawi

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Msaidizi anayeshughulika na Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Luteni Kanali Selestine Masalamado ameongoza ujumbe wa kutoka Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kupeleka misaada ya unga, mahindi, mablanketi, mahema na madawa mbalimbali ambayo yatasaidia waathirka wa Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi.
Magari ya Jeshi la wananchi Tanzania yaliyobeba Vifaa Mbalimbali vya Msaada wa Kibinadamu yakivuka Mpaka kuelekea jijini Blantyre. 

Luteni Kanali Masalamado amesema hayo Machi 22, 2023 wakati msafara wa magari ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania yakivuka mpaka wa Kasumulu Wilaya ya Kyela kuelekea Mji wa Blantyre nchini Malawi.
“Natoa pole kwa ndugu zetu, wananchi wa Malawi tuko nao katika hali hii ngumu,”amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi, Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Luteni Kanali Selestine Masalamado (katikati) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Karonga nchini Malawi,Roderick Mateauma. 

“Katika kuitikia hilo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya majanga,”amesema.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyela,Godfrey Kawacha akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karonga nchini Malawi, Mhe. Roderick Mateauma (kulia) kabla ya magari yaliobeba misaada ya kibinadamu ya kuvuka Mpaka wa Kasumulu kuelekea jijini Blantyre Malawi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wlaya ya Karonga nchini Malawi, Mhe. Roderick Mateauma ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kwamba msaada huo utasaidia kupunguza athari kwa wahanga na inaonesha mahusiano ya karibu yalipo kati ya nchi hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news