MIWILI YAKE SAMIA-4: Amethibitishia inawezekana

NA LWAGA MWAMBANDE

MHESHIMIWA Dkt.Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya miaka miwili amefanikiwa kuiongoza nchi kwa umahiri mkubwa na kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano kwa Watanzania.

Vivyo hivyo, imekuwa ni miaka miwili ya mafanikio, matumaini, faraja na matarajio makubwa kwa Watanzania kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Serikali na ushirikiano mkubwa ambao Serikali imeupata kutoka kwa wananchi.

Watanzania wameshuhudia utekelezaji wa kasi wa miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya kimkakati kwa Taifa letu inayojumuisha ujenzi reli ya kisasa, miradi ya umeme,usafirishaji wa majini, nchi kavu na angani,ujenzi wa ofisi za Serikali makao makuu Dodoma na uwekezaji katika maeneo mbalimbali.

Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasema, miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt.Samia, miradi mingi ikiwemo ile ya kimkakati imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa kasi kwa manufaa ya Watanzania na Taifa. Endelea;

74.Miradi ya Tanzania,
Mikubwa kuisikia,
Inazidi kuvutia,
Heko Rais Samia.

75.Reli mpya kianzia,
Dasalamu yaanzia,
Mwanza ndiko taishia,
Heko Rais Samia.

76.Dar-Moro nakwambia,
Pazuri imefikia,
Na hadi Dodoma pia,
Heko Rais Samia.

77. Tutaanza kutumia,
Reli tukisafiria,
Mwendokasi nakwambia,
Heko Rais Samia.

78. Vipande vitano pia,
Vyote kazi meingia,
Hadi kuimalizia,
Heko Rais Samia.

79.Umetuthibitishia,
Kwamba unafwata njia,
Maneno matendo pia,
Heko Rais Samia.

80.Ulikwishatuambia,
Wakati lipoingia,
Miradi kuhudumia,
Heko Rais Samia.

81.Reli hiyo yaingia,
Mabehewa mesikia,
Ni kazi kuyatumia,
Heko Rais Samia.

82.Huduma twasubiria,
Zile zinazovutia,
Kwetu sisi abiria,
Heko Rais Samia.

83.Umeme zigo sikia,
Mradi wa Tanzania,
Mkubwa ninakwambia,
Heko Rais Samia.

84.Magufuli lianzia,
Kazi ilipoanzia,
Tunazidi furahia,
Heko Rais Samia.

85.Hatua liyofikia,
Bwawa tunajijazia,
Huku tunaangalia,
Heko Rais Samia.

86.Lengo ni kumalizia,
Umeme weze ingia,
Nasi tuweze tumia,
Heko Rais Samia.

87.Mradi kumalizia,
Sote tutafurahia,
Kwa umeme Tanzania,
Heko Rais Samia.

88.Maji ndiyo yaingia,
Bwawa yanatujazia,
Hadi lengo kutimia,
Heko Rais Samia.

89.Mradi ukitimia,
Ni umeme mwingi pia,
Kutumia Tanzania,
Heko Rais Samia.

90.Si umeme twatambia,
Kwamba tutafurahia,
Mengi tunafurahia,
Heko Rais Samia.

91.Kama Reli Tanzania,
Na umeme Tanzania,
Ajira zinaingia,
Heko Rais Samia.

92.Mafundi kuhudumia,
Kazi wakitufanyia,
Uchumi unaingia,
Heko Rais Samia.

93.Hapohapo ingizia,
Bomba la mafuta pia,
Uganda to Tanzania,
Heko Rais Samia.

94.Maneno yalianzia,
Mipango ikafwatia,
Mradi tutimizia,
Heko Rais Samia.

95.Pale umeshikilia,
Vitendo kutufanzia,
Kazi kazi nakwambia,
Heko Rais Samia.

96.Wajenzi wameingia,
Kazi wanatufanyia,
Wamo na Watanzania,
Heko Rais Samia.

97.Saruji wanatumia,
Viwanda vya Tanzania,
Na hata mabomba pia,
Heko Rais Samia.

98.Chakula wanatumia,
Kile tunajilimia,
Mapesa yanaingia,
Heko Rais Samia.

99.Kote wanakopitia,
Wameshapata fidia,
Faida kwa Tanzania,
Heko Rais Samia.

100.Haya tunaangalia,
Wengi tunafurahia,
Uchumi unaingia,
Heko Rais Samia.

101.Wengine wanasinzia,
Kazi kulalamikia,
Makosa kutafutia,
Heko Rais Samia.

102.Wako wanaoumia,
Ya Uganda Tanzania,
Kwao hayajaingia,
Heko Rais Samia.

103.Lakini twafurahia,
Serikali zetu pia,
Mradi kushikilia,
Heko Rais Samia.

104.Hoima unaanzia,
Uganda kule sikia,
Hadi Tanga kuishia,
Heko Rais Samia.

105.Kote bomba lapitia,
Faida linaachia,
Uchumi twafurahia,
Heko Rais Samia.

106.Tanga litapofikia,
Mafuta safirishia,
Tutazidi shangilia,
Heko Rais Samia.

107.Tanga kutuinulia,
Uchumi ulosinzia,
Na bandari yetu pia,
Heko Rais Samia.

108. Wagosi wa Tanzania,
Biashara furahia,
Huduma kutupatia,
Heko Rais Samia.

109.Hapohapo mesikia,
Mradi mwingine pia,
Bomba la gesi sikia,
Heko Rais Samia.

110.Dasalamu kuanzia,
Na Mombasa kuishia,
Hilo twalisubiria,
Heko Rais Samia.

111.Hii ni neema pia,
Kwetu sisi Tanzania,
Mapato yataingia,
Heko Rais Samia.

112.Gesi yetu asilimia,
Pesa tutajipatia,
Na mengine mengi pia,
Heko Rais Samia.

113.Mradi kufungulia,
Fursa zitaingia,
Maisha tafurahia,
Heko Rais Samia.

114.Ajira zitaingia,
Huduma kuwapatia,
Na bidhaa zetu pia,
Heko Rais Samia.

115.Inanoga Tanzania,
Fursa kuzitumia,
Uchumi kujikuzia,
Heko Rais Samia.

Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news