MWANAKWEREKWE INAKWENDA MAITI

NA ADELADIUS MAKWEGA

MWANAKWETU alishuka katika boti Forodhani Zanzibar na kutembea kwa miguu mwendo kidogo kuvuka uzio wa forodha hii, huku akipishana na magari mengi yaliyofika hapo kuwapokea abiria hao. Kwa hakika mwanakwetu alitamani apate bahati ya kupokelewa na Wazanzibari, lakini Mungu bahati hiyo hakumjali ndugu yetu huyu. 
Aliendelea kutembea na mbele yake alikuwepo kijana mmoja, alimshika bega na kumuomba msamaha, alimsalimu alafu alimuuliza eti Mwanakwerekwe ni wapi?. 

Kijana huyu alijibu kuwa na hata yeye si mwenyeji Zanzibar, mwanakwetu alimvuka kijana huyo na pia kuivuka barabara na kumfuata mfanyabiashara mmoja aliyekuwa kando ya biashara yake.Habari ndugu?. Samahani nakwenda Mwanakwerekwe, lakini sipafahamu. Ndugu huyu alimcheka mwanakwetu alafu akamuuliza kaka unakwenda Mwanakwereke? Wewe maiti? 

Mwanakwetu ajibu naam mimi ni maiti tarajiwa. Jamaa huyu akacheka zaidi halafu akamuuliza ehee unakwenda Mwanakwereke kufanya nini? Mwanakweti akajibu kuwa anakwenda kuposa, jamaa huyu akasema kwa kuwa unakwenda kuposa dada zangu wewe ni ndugu yangu ngoja nikuelekeze. 

“Nenda na barabara hii moja kwa moja hadi mataa, alafu kata kulia alafu tembea hadi mataa ya pili, alafu kata kushoto, utakutana na maghorofa ya serikali marefu sana hapo utaona basi zimesimama zinaanzia namba 500 wewe panda 510 utafika Mwanakwerekwe.” 

Msomaji wangu nakupa siri moja kubwa mwanakwetu ni bingwa kukariri mno, aliyafuata maelekezo hayo hatua kwa hatua, kweli alijikuta amefika maghorofa marefu na kupata hiace yenye nambari 510 na kuingia ndani yake kuanza safari huku akimuomba dereva wa hiace hiyo amshushe Mwanakwerekwe jirani na mahakama. 

Dereva wa Hiace ambaye alionekana mtu mwema sana akasema pale Mwanakwerekwe kuna mahakama mbili Mahakama Kufungwa na Mahakama Mapenzi, wewe unakwenda mahakama ipi?Mwanakwetu akajibu kwa kubabia, mie nakwenda Mahakama Mapenzi, Dereva akacheka sana, alafu akasema kule kaka wanaokwenda mara nyingi kushitaki ni wanawake sie wanaume japokuwa tuna haki zetu sijawahi kuona tunakwenda huko. Mwanakwetu akajibu kuwa yeye atakuwa wa kwanza. 

“Pale utasikia mie mtoto wangu hatunzwi, mie naonba taraka, mie kagoma kutunza ujauzito.” 

Mwanakwetu akarudia mara ya pili maneno haya, “Leo hii nitakuwa mwanaume wa kwanza kushitaki katika Mahakama Mapenzi ya Mwanakwerekwe.” Abiria ndani ya Hiace wanacheka. 

Akiwa ndani ya Hiace hiyo mwanakwetu alikumbuka lile neno aliloambiwa pale Forodhani juu ya wanaokwenda Mwanakwerekwe mara nyingi ni maiti, akasema aulize maana yake nini? 

“Unajua mwanakwerekwe kuna makaburi ya watu wote, uwe mwenyeji, uwe mgeni au mtu aliyejifia tu, huko maiti yake inabebwa hadi Mwanakwerekwe na kuzikwa bila shida.” 

Maelezo haya mwanakwetu aliiambiwa na dereva huyu huku safari inasonga na mara kondakta aliomba naulil yake naye mwanakwetu akatoa shilingi 1000/- na kurudishiwa shilingi 500/- alafu mwanakwetu akashuka huku dereva huyu akimuelekeza sehemu aliyokuwa anakwenda.
Kweli aliposhuka mwanakwetu alipita mtaa mmoja na akakutana na jengo moja nzuri la ghorofa lililokuwa na maandishi haya SMZ, Dr. John P. Magufuli Secondary School-Zanzibar.

Mwanakwetu yu Zanzibar aliyakumbuka mambo makubwa matatu Kwanza;-Unakwenda Mwanakwerekwe wewe maiti? Pili- Unakwenda Mahakama Kufungwa au Mahakama Mapenzi? na Tatu, Ghorofa zuri lenye maandishi ya SMZ, Dr. John P. Magufuli Secondary School Zanzibar. 

Msomaji wangu wewe kazi kwako kuchagua moja kati ya hayo matatu. Mwanakwetu kachagua Unakwenda Mwanakwerekwe wewe maiti? Wewe unachagua lipi? 

Nakutakia siku njema. 
0717649257

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news