Nabii Tshibangu kutoka Afrika Kusini aungana na Rais Dkt.Nabiijoshua kuwakaribisha watumishi wote kwenye Kongamano la Kitaifa la Mashangilio

NA DIRAMAKINI

MWANGALIZI Mkuu wa Huduma ya Neno la Uzima (Eternal Word Ministries) nchini Afrika Kusini, Nabii Christian Binene Tshibangu ameungana na Rais wa Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania (UMMT), Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala kuwakaribisha watumishi wote wa Mungu kupitia huduma tano katika Kongamano la Kitaifa la Mashangilio ambalo litafanyika Aprili 1, 2023. Huduma tano zinajumuisha Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Walimu.

Rejea neno la Mungu kupitia Biblia Takatifu, Waefeso 4:11-12...11 Yeye ndiye aliyewapa watu vipawa, wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na walimu; 12 wapate kuwatayarisha watu wa Mungu kwa kazi za huduma, kwa ajili ya kujenga kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo. 
Nabii Tshibangu ametoa wito huo leo Machi 28, 2023 ikiwa ni siku chache zimesalia kabla ya kufanyika kongamano hilo la kihistoria katika Ukumbi wa Ubungo Plaza uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

"Kuna mitume, walimu, madaktari, wainjilisi, walimu na wachungaji ambao tayari wameshaungana,vipi kuhusu wewe? Sisi manabii ambao tupo nje ya Tanzania, tumeelewa maono, dhamira na kazi ya Umoja wa Mitume na Manabii,na tunaungana nao kwa pamoja na Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania kwa hatua hii muhimu ya majumuiko katika kuujenga mwili wa Kristo...

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news