Rais Dkt.Samia aunda kamati kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje, afanya uteuzzi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha wizara hiyo kutekeleza malengo ya Serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.
Ili kutekeleza azma hiyo amemteua Balozi Yahya Simba, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia kuwa Mwenyekiti wa Kamati. Aidha, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati:

Balozi Ramadhan Mwombe Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mstaafu;

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus wengine ni Balozi Dkt. Mwanaidi Sinare Maajar, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

Balozi Peter Allan Kallaghe, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza; na Balozi Tovako Nathaniel Manongi, aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Kamati hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 31 Machi, 2023 Ikulu Dar es Salaam, saa 08:30 mchana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news