Rais Dkt.Mwinyi ashiriki mazishi ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile

Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakibeba mwili wa marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile kwa ajili ya kuswaliwa sala ya maiti katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi Machi 3, 2023.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi (wa tano kulia) akijumuika na viongozi mbalimbali na wananchi katika kumswalia marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile, katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi..
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab (wa pili kushoto) akijumuika na Waislamu wengine kuupokea mwili wa Marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile, katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi kwa ajili ya swala maiti. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimpa mkono wa pole Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe.Zubeir Ali Maulid mara baada ya sala ya Maiti kumswalia Marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile, katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemedi Suleiman Abdulla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na viongozi baada ya Swala ya Ijumaa na kuswalia Mwili wa marehemu Habibu Ali Mohamed aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile, katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi.

Post a Comment

0 Comments