Rais Dkt.Nabiijoshua atakuwepo Ubungo Siku ya Mashangilio

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania (UMMT), Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala amesema, Aprili Mosi, mwaka huu ambayo itakuwa ndiyo Siku ya Kitaifa ya Kongamano la Mashangilio litakalofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam,atakuwepo.

Ubungo Plaza panatajwa kuwa ni mahali pazuri sana kusherehekea hafla nyakati zote kwa sababu iko katikati ya jiji, na mawasiliano mazuri, maegesho, lifti na huduma zingine ambazo husaidia kuwezesha kila kitu unachohitaji kufurahia wakati wako.
Hivi karibuni,Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania alitwaa asilimia 80 ya kura katika uchaguzi wa nafasi ya urais katika Umoja wa Manabii na Mitume nchini Tanzania (Unity of Apostles and Prophets Tanzania).

Ushindi huo ulitokana na kura 179 alizopata huku akiwaacha mbali washindani wake akiwemo Mchungaji Ceasar Masisi aliyepata kura 42 na Mtume Joackim Kimanza aliyepata kura nne kupitia uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Anatoglo uliopo Ilala, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Askofu Profesa Rejoice Ndalima alimtangaza rasmi Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala kuwa Rais wa Umoja wa Mitume na Manabii nchini Tanzania.

Aidha, mitume na manabii mbalimbali nchini walionesha imani kubwa juu ya Dkt.Nabiijoshua huku wakimpongeza na kuahidi kumpa ushirikiano mkubwa aweze kutekeleza jukumu lake la kuwaunganisha viongozi hao wa kiroho ili waweze kulihubiri neno la Mungu kwa ufanisi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news