Rais Dkt.Samia aahidi mema zaidi nchini

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wanawake kupaza sauti kwa pamoja na kukemea changamoto zinazowakabili wanawake wa Tanzania katika nyanja mbalimbali bila kujali itikadi zao. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda kabla ya kuhutubia Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita kwenye Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu).

Rais Dkt.Samia ametoa wito huo leo Machi 19, 2023 wakati akihutubia katika sherehe ya kilele cha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru.
Aidha, Rais Dkt.Samia ameahidi kuendelea kutafuta suluhu za changamoto zinazowakabili wanawake na kuwafanya kukosa huduma ikiwemo kujenga shule za wasichana za sayansi na vyuo vya ufundi ili kuwainua wanawake katika masuala ya kiteknolojia. 

Kwa upande wa miundombinu, Rais Dkt.Samia amesema Serikali imeweka bajeti ya kutosha kuiwezesha Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuendeleza miundombinu ya barabara vijijini. 
Vile vile, Rais Dkt.Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha Bandari za Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Mtwara na Kigoma ili kuimarisha biashara nchini na ndani ya bara la Afrika kwa ujumla. 

Halikadhalika, Rais Dkt.Samia amesema Serikali itasimamia Tanzania kuwa kinara wa uchumi kwa kumsimamia mwanamke kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazouzwa ndani na nje ya nchi kama ilivyopendekezwa na Jukwaa la Usawa wa Kijinsia. Rais Samia pia ameeleza kuwa changamoto za mabadiliko ya tabia nchi zimesababisha kupanda kwa gharama za bidhaa hivyo, Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto hizo kuhakikisha Watanzania wanakuwa na ustawi mzuri wa maisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news