Rais Dkt.Samia apokea ripoti ya TAKUKURU,CAG

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi na watendaji wa Serikali kuzisoma na kuzielewa vyema taarifa za rushwa na za ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ziwasaidie kujitathmini. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Machi 29, 2023.(Picha na Ikulu).
Rais Dkt.Samia ametoa agizo hilo leo mara baada ya kupokea taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika hafla iliyofanyika Ikulu. 

Aidha, Rais Samia amesema taarifa hizo hizo zinasaidia kusimamia na kuimarisha utawala bora na kuhakikisha udhibiti na usimamizi wa rasilimali za Serikali unafanywa kikamilifu. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2021/2022 kutoka kwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo, CP. Salum Hamduni Ikulu jijini Dar es Salaam leo Machi 29, 2023.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Samia ameitaka Mamlaka ya Bandari kufanya kazi na sekta binafsi ili kuimarisha mifumo ya TEHAMA ya ukusanyaji fedha ambapo itasaidia kudhibiti upotevu mkubwa wa fedha unaotokea bandarini. 

Rais Samia pia amegiza kufanyiwa tathmini kwa Mashirika ya Umma yaliyopata hasara na kuyafuta Mashirika ambayo hayana tija kwa taifa kwa kuwa Mashirika hayo yanatumia gharama kubwa lakini hayaleti faida kwa Serikali. 
Katika ripoti ya CAG jumla ya Halmashauri 14 nchini zimepata hati zenye mashaka zikiwemo Halmashauri ya Jiji la Arusha, Babati, Bahi, Geita, Kilindi, Mbinga, Musoma, Nkasi, Nyasa, Simanjiro, Songwe, Sumbawanga Manispaa pamoja na Ushetu iliyopata hati mbaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news