Rais Dkt.Samia aunda Baraza la Kumshauri kuhusu Utekelezaji wa Masuala ya Kilimo na Chakula, afanya uteuzi

NA DIRAMAKINI

KATIKA kutekeleza azimio la Viongozi wa nchi za Afrika, kupitia Mkutano wa Utoshelevu na Ustahimilivu wa Chakula (Dakar 2 Summit on Feed Africa: Food Sovereignty and Resilience) uliofanyika Dakar, Senegal tarehe 25 - 27 Januari, 2023, waliazimia kila nchi kuunda Mabaraza ya kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kukuza kilimo na kuongeza uzalishaji wa chakula (Presidential Food and Agriculture Delivery Council). Ili kufikia azma hiyo;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Baraza la Kumshauri Rais kuhusu Utekelezaji wa Masuala ya Kilimo na Chakula (Presidential Food and Agriculture Delivery Council); na amemteua Mhe. Mizengo Kayanza Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Aidha, Mhe. Rais amewateua Bw. Geoffrey Kirenga, Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT na Bw. Andrew Masawe, Katibu Mkuu Mstaafu kuwa Wajumbe wa Baraza hilo.

Vile vile Mheshimiwa Rais, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Baraza: -

1:Dkt. Florence Turuka, Katibu Mkuu Mstaafu na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA);

2:Dkt. Jacqueline Mkindi, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticulture Association (TAHA); na

3:Dkt. Mwatima Juma, Mwenyekiti wa Tanzania Organic Agricultural Movement (TOAM).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi,Zuhura Yunus leo Machi 14, 2023 baraza hilo litazinduliwa tarehe 17 Machi, 2023 Ikulu, Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news