TAEC chini ya uongozi wa Prof.Busagala yarekodi mafanikio ya aina yake Tanzania

NA DIRAMAKINI

TUME ya Nguvu za Atomu Tanzania (Tanzania Atomic Energy Commission-TAEC) chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu, Prof.Lazaro S.P.Busagala imerekodi mafanikio makubwa kuanzia Machi 2018 hadi Februari, 2023.
TAEC ilianzishwa kwa Sheria ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Na.7 ya mwaka 2003 (The Atomic Energy Act, No. 7 of 2003). 

Sheria hii ya Bunge Na. 7 ya mwaka 2003 ilifuta Sheria Na.5 ya mwaka 1983 (The Protection from Radiation, No. 5 of 1983) iliyoanzisha Tume ya Taifa ya Mionzi (National Radiation Commission).

TAEC ina majukumu mawili makubwa ikiwemo kudhibiti matumizi salama ya mionzi, na pili ni kuinua matumizi salama ya sayansi na teknolojia ya nyuklia. 

Kwa upande wa udhibiti wa matumizi salama ya mionzi. TAEC inasajili na inatoa leseni kwa wale wote wanaomiliki vyanzo vya mionzi baada ya kuti miza masharti ya kiusalama wa mionzi na nyuklia. 
Kusudi la kufanya kazi hizi ni kuwaweka watanzania katika hali ya salama dhidi ya madhara ya mionzi ambayo yanayoweza kujitokeza. 

Faida ya udhibiti wa viwango vya mionzi ni kulinda afya za watanzania, mazingira na soko la bidhaa za Tanzania zinazo safirishwa nje ya nchi.

Tume inafanya nini?

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Peter Ngamilo amesema, TAEC inatekeleza kazi mbalimbali katika kuhakikisha kuwa inatimiza majukumu makuu iliyopewa na malengo ya kuundwa kwake.
Ngamilo amesema, kazi hizo ni pamoja na kutoa vibali vya uingizaji, umiliki, usafirishaji na utumiaji wa vyanzo vya mionzi hapa nchini.

Pia kukagua vituo vyote vyenye vyanzo vya mionzi ili kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Nguvu za Atomu na kanuni zake.

Tatu,kupima sampuli za vyakula, mbolea, vyakula vya wanyama, tumbaku na mazao yake vinavyoingizwa nchini na kusafirishwa nje ya nchi ili kuweza kudhibiti hatari ya athari ya mionzi.

Nne, kupima sampuli za mazingira ili kubaini uchafuzi wa mionzi kwenye mazingira, na tano ni kupima kiwango cha mionzi kwenye minara ya simu na rada za mawasiliano.

Sita ni kukusanya, kusafirisha na kuhifadhi mabaki vyanzo vya mionzi huku saba ikiwa ni kutoa huduma ya upimaji wa mionzi kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye maeneo yenye vifaa vya mionzi.
Nane ni kuendesha kituo cha kupima uchafuzi wa anga (Air Pollution) unaotokana na majaribio ya silaha za nyuklia (Radionuclides Monitoring Station- RN64).

Tisa ni kuratibu miradi mbalimbali ya matumizi ya teknolojia ya nyuklia hapa nchini, jukumu la 10 ni kutoa elimu kwa umma juu ya faida na madhara ya teknolojia ya nyuklia.

Mengine ni kuendeleza tafiti za teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii ikiwemo kutoa huduma za matengenezo ya vifaa vinavyotumia teknolojia ya nyuklia kama vile X-Ray, CT-Scan.

Miradi

Katika kuhamasisha na kuinua matumizi salama ya sayansi na teknolojia ya nyuklia, TAEC huratibu miradi mbalimbali ya kitaifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo mbalimbali hasusani Shirika la Nguvu za Atomu la Kimataifa (IAEA) na Umoja wa Ulaya. Miradi mbalimbali imeleta matokeo chanya kwenye sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, afya, maji, na mifugo.

Aidha, kuna mafanikio na mwenendo chanya wa TAEC kwa ujumla hadi Februari 2023 chini ya uongozi wa Prof. Lazaro S.P. Busagala aliteuliwa Machi 22, 2018. Uteuzi huo ulifanyika baada ya kuwa na sitonfahamu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu hivi. 

Mafanikio yaliyopatikana

Chini ya uongozi wa Prof.Busagala, mafanikio ya TAEC ambayo yamepatikana ni mengi ikiwemo kurejesha utulivu, amani, maelewano kati ya watumishi wa TAEC na menejimenti kwa njia mbalimbali.
Miongoni mwa njia zilizotumika ni kufanya vikao mara kwa mara na watumishi wote pamoja na Mkurugenzi Mkuu ili kuwasikiliza na kuchukua mapendekezo yao yanayo tekelezeka. 

Jambo hili linasaidia kuhakikisha kutatua changamoto au malalamiko ambayo yangeleta shida kama yasinge shughulikiwa mapema. 

Njia nyingine ni kutumia vyombo vya maamuzi kama vile vikao vya Menejimenti, Bodi na Kamati zake ikiwemo kuruhusu vyombo vya wafanya kazi vilivyopo kisheria kufanya kazi zake bila kubughudhiwa.

Sambamba na kushirikisha watumishi katika maamuzi kwa njia zilizopo. Kauli mbiu ya KKN ambayo maana yake ni Kazi kwa Kasi na Nidhamu imekua shirikishi na wafanyakazi wameipokea kwa nia moja ya kuondoa matabaka na kuleta kuheshimiana na kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu. Pia, kumekua na kuthamini michango ya kila mmoja wao katika tume. 

Aidha, chini ya uongozi wa Prof.Busagala, tume imekuwa ikiwasogezea wananchi huduma kwa njia ya kuanzisha na kuendelea kusimamia ujenzi wa miundombinu inayoipa TAEC uwezo wa kutoa huduma. 

Katika hili majengo sita ya maabara mbambali, ofisi na mitambo mingine kwa mafanikio imejengwa kwa mafanikio na iko kwenye hatua mbalimbali. 

Miradi hiyo ipo Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Zanzibar ili kutoa uwezo wa kuwahudumia wananchi na ukarabati wa miundo mbinu husika. Linaonesha hali iliyokuwepo kabla yake na hali ya sasa. 

Kwa kina

Chini ya uongozi wa Prof.Busagala, TAEC imeanzisha na kuendelea kutekeleza kwa mafanikio miradi hiyo ambapo iko kwenye hatua mbalimbali hadi kufikia Februari 20, 2023 na imegharimu zaidi ya shilingi bilioni 28.77.

Tukianzia na mradi wa Maabara Changamano ambao upo jijini Arusha huu umegharimu shilingi bilioni 10.45 ambapo hadi Machi 23, 2018 haukuwepo ingawa michoro ilikuwepo tangu mwaka 2012 na hadi kufikia Februari 20, 2023 umekamilika kwa asilimia 100.

Mradi mwingine ni wa Maabara na Multipurpose Irradiator ambao unatekelezwa kwa thamani ya shilingi bilioni 7.9 jijini Dar es Salaam, mradi huu hadi Machi 23, 2018 haukuwepo, lakini hadi kufikia Februari 20, 2023 umefikia asilimia 34.

Pia, kuna mradi wa Maabada na Ofisi jijini Dodoma ambao umegharimu shilingi bilioni 3.8 ambapo hadi Machi 23, 2018 haukuwepo katika mipango, lakini hadi kufikia Februari 20, 2023 mradi umekamilika kwa asilimia 100.

Aidha, kuna Maabara na Kituo cha Utafiti jijini Dodoma ambapo thamani ya mkataba ya ujenzi bado haijajulikana, na hadi kufikia Machi 23,2018 haukuwepo katika mipango, lakini hadi kufikia Februari 20,2023 tayari kiwanja na hati zipo huku michoro ikiandaliwa.

Kwa upande wa Jiji la Mwanza, TAEC inatekeleza mradi wa Maabara na Ofisi ambao una thamani ya shilingi bilioni 2.85 ambapo hadi kufikia Machi 23, 2018 haukuwepo, lakini hadi kufikia Februari 20, 2023 umefikia asilimia 90.
TAEC, pia kwa upande wa Zanzibar inatekeleza mradi wa ujenzi wa Maabara na Ofisi ambao unagharimu shilingi bilioni 3.03 hadi kufikia Machi 23, 2018 haukuwepo, lakini kwa sasa mradi huo kufikia Februari 20, 2023 umefikia asilimia 75.

Miradi mingine ni ukarabati wa majengo sita ya nyumba za watumishi, mabaki ya mionzi na utawala kwa gharama ya shilingi milioni 360.21 ambapo hadi kufikia Machi 23, 2018 haukuwepo, lakini hadi Februari 20, 2023 mradi umekamilika kwa asilimia 100.

Jijini Arusha, pia tume imetekeleza mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo (netball, basketball, football) na chumba cha kubadilishia nguo kwa thamani ya shilingi milioni 140.91 ambapo hadi kufikia Machi 23, 2018 haukuwepo, lakini hadi Februari 20, 2023 umekamilika kwa asilimia 100.

Mradi mwingine ni ujenzi wa uzio, Block D, Njiro jijini Arusha kwa gharama ya shilingi milioni 183.56 ambapo hadi kufikia Machi 23, 2018 haukuwepo, lakini hadi Februari 20, 2023 mradi umekamilika kwa asilimia 100.

Wakati huo huo, TAEC imepiga hatua kubwa katika kutafuta na kupata viwanja vya ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama vile maabara za kanda Dar es Salaam (40,000 mita mraba), Dodoma (15,625 mita mraba), Mbeya (11,488 mita mraba), Mwanza (8,730 mita mraba), na Zanzibar (7,314 mita mraba).

Kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (CAG) kwa miaka yote tangu 2017/2018 hadi sasa. 
Uongozi wake, ulipoanza Aprili 2018, uliitisha ukaguzi maalum na hatua sitahiki kuchukuliwa. Hatua hizo zilisaidia kuepuka kupata hati chafu ambayo ingeleta picha mbaya kwa Serikali.

Chini ya uongozi wa Prof.Busagala, tume imefanikiwa kuongeza makusanyo ya maduhuli ya serikali kwa asilimia 260 ikiwa ni kutoka shilingi bilioni 2.8 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hadi kufikia shilingi bilioni 10.09 mwaka fedha 2021/2022 baada ya kuchukua hatua mbalimbali kama vile kufungua ofisi za mipakani na kutumia mifumo ya TEHAMA kama vile TANCIS, TeSWS na EDMS.

Tume pia imefanikiwa kuboresha mazingira ya biashara kwa kupunguza muda wa utoaji wa vibali kwa wanaoingiza na kusafirisha mizigo inayodhibitiwa na TAEC. 

Awali utaratibu wa utoaji vibali ulikuwa una mlolongo mrefu ambao ulisababisha malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali. 
Kitendo hiki kilipelekea TAEC kupata lawama za wadau mbalimbali na kuwa miongoni mwa taasisi zinazokwamisha biashara. 

Utaratibu wa utoaji vibali ulibadilishwa kwa kupunguza mlolongo usio wa lazima pamoja na kutumia zaidi mfumo wa electroniki kupunguza muda na kuongeza ufanisi. 

Hatua hizi zimeongeza ufanisi kwa kupunguza siku za utoaji wa vibali kutoka zaidi ya siku 7 hadi kufikia siku moja (98%). Mfumo wa ki-electronik husaidia kutoa vibali ndani ya saa tatu.

Nyingine ni kuboresha mazingira ya biashara kwa kupendekeza punguzo la tozo. Hii ilifanyika kwa kuboresha kanuni za tozo hivyo kupunguza gharama za biashara hasa kwa wale wanaosafirisha bidhaa nje ya nchi kwa kupunguza kutoka asilimia 0.2 ya malipwani kuwa asilimia 0.1 ya malipwani.

TAEC imefanikiwa kuweka mpango mkakati wa miaka mitano (2018/2019-2022/2023), kisha wa miaka mitatu (2022/2023 - 2025/2026) na kutekeleza kwa mafanikio kiasi cha kuvuka malengo ya mipango kazi kila mwaka hata baada ya kuongeza malengo kila mwaka unaofuata. 
Hili limewezekana kwa kupitia mifumo ya majukwaa mbalimbai ya usimamizi wa kazi na ufuatiliaji wa kazi. Mfano jukwaa la kuripoti kazi za kila wiki, jukwaa na vikao vya kufuatilia mpango kazi kwa kila wiki (Four Disciplines of Excution (4DX)). Yote haya yameongeza uawajibikaji wa watumishi na kuongeza ufanisi kazini. 

Aidha, kuongeza na kuboresha matumizi ya TEHAMA kuanzia tovuti ya tume. Hii ina mchango mkubwa sana katika mafanikio mengi yalielezewa hapa. 

Uongozi wa TAEC uliboresha matumizi ya email za serikali, GePG, TANCIS, TeSWS. Haya yote yamekuza mawasiliano ndani na nje ya TAEC na kuleta matokeo chanya katika maeneo mbalimbali. 

Pia kutengeneza mfumo wa “Electronic Document Management System-EDMS” ambao hutumika kuchakata vibali mbalimbali ikiwa pamoja na kuchakata maombi mbalimbali ya malipo, likizo na mambo mengine. EDMS ina mchango mkubwa sana katika suala la kuongeza maduhuli ya serikali. Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na:

Hii imefanyika kwanza kwa kufanya usajili wa tovuti ya tume na kutumia www.taec.go.tz kama ulivyo mwongozo kutoka Ofisi ya Rais Utumishi. 

Tovuti ya Tume imekua ofisi ya mtandaoni, ikitoa taarifa za muda huu (up to date) za Tume kwa wadau wake pamoja na kutoa fursa ya kupata fomu na nyaraka mbalimbali bila kuhitaji kufika ofisini.

Pia kuwatengenezea watumishi anuani za barua pepe za serikali ambapo kabla ya Aprili 2018 hazikuwepo. Jambo hili limeleta mafanikio makubwa kwenye kurahisisha mawasiliano na kuongeza ufanisi miongoni mwa watumishi. 

Na hivyo kwa barua pepe moja watumishi wote wanaweza kufikiwa. Hii pia inaokoa gharama za kudurufu vitini na hati mbalimbali vya vikao na mambo yanayofanana na hayo. 

TAEC imeanza kutumia GePG mwaka 2018, kwa makusanyo ya maduhuli hivyo kuweza kutoa risiti za electronic. Ununuzi wa mashine za POS (point of sale) kwa ajili ya ofisi za mipakani imefanywa na kuimarisha kazi za Tume katika mipaka ya nchi.

Mfumo wa kuchakata vitini na hati mbalimbali (EDMS) ikiwemo vyeti vya uchunguzi vya mionzi ukaaanza kutumika baada ya ofisi ya GePG kuidhinisha kwa kukidhi viwango.

Kuunganisha mifumo ya TEHAMA na TANCIS, kisha TeSWS jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa katika kudhibiti matumizi salama ya mionzi ikiwemo kuongeza makusanyo ya maduhuli ya serikali. 

Mafanikio mengine ni kuongeza watumishi wa kudumu kutoka 89 hadi kufikia 134. Juhudi kubwa ilihitajika kuweza kujenga hoja na kupata vibali vya kuajiri. Juhudi zinaendelea ili kuondosha pengo ambalo bado lipo.

Mengine ni kutatua tatizo la kupandishwa vyeo na mishahara kwa baadhi ya watumishi lililodumu kwa muda mrefu bila kutatuliwa kwa kupanda madaraja (promotion). 

Kulikuwa na watumishi wasiopungua 57 wa TAEC ambao mishahara na vyeo vyao vilikuwa na matatizo yaliyodumu kwa muda mrefu na baada ya ufuatiliaji wa karibu, wafanyakazi walipata stahiki zao.

Sambamba na kuwajengea uwezo watumishi ili wawe na utendaji wenye weledi kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi wasiopungua 31 na wale walihudhuria semina wasiopungua 100 kwa kila mwaka.

Aidha, kuwajengea uwezo wa kitaalam watumishi ili kujenga taifa lenye uwezo katika teknolojia ya nyuklia. Hivyo mpango wa mafunzo uliwekwa na kuanza kutekelezwa. 
Hili ni muhimu sana kwa ustawi wa taifa letu katika sekta ya sayansi na teknolojia ya nyuklia. Hatua hii iliongeza idadi ya watumishi waliojiunga na masomo katika ngazi mbalimbali (astashahada, stashahada, shahada, shahada za uzamili na uzamivu) kutoka 7 hadi kufikia 24 mwezi Juni 30, 2022. Katika hao waliongezeka 21 wamepewa ufadhili na TAEC kwa asilimia 100.

Kutekeleza mpango wa kuanzisha Ufadhili wa vijana watano kila mwaka chini ya Ufadhili wa Mhe. Samia Suluhu Hassan (H.E. Samia Suluhu Hassan Scholarship) kwa wale wanaofanya vizuri zaidi katika nyanja za kinyuklia. 

Lengo la mpango huu ni kuhakikisha nchi inajenga uwezo wa kufanya makubwa zaidi katika sekta ya teknolojia ya nyuklia. 

Ili kuboresha utendaji na kufikia lengo la utekelzaji wa mipango mbalimbali, na ili kukabiliana na kupanuka kwa kazi na majukumu, TAEC imenunua magari mapya saba ndani ya miaka minne. Suala hili limeiongezea TAEC uwezo wa kukagua hivyo kuwaweza watanzania na mazingira katika hali ya usalama zaidi.

Kubuni na kutengeneza gari maalum la kubebea vyanzo vya mionzi. Katika kipindi cha muda mrefu, watumishi wa TAEC walikuwa wakitumia mbinu za zamani zisizokuwa salama za usafirishaji wa vyanzo vya mionzi ambapo watumishi na vyanzo vya mionzi kwa pamoja hukaa katika gari moja linalotenganishwa na vifaa maalumu. 

Jambo hili lilikuwa linalalamikiwa na kutia mashaka juu ya usalama wa watumishi wanaosafirisha vyanzo vya mionzi. Kwa sababu ya usikivu wa Mkurugenzi Mkuu na manejimenti yake waliamua kubuni na kuunda gari kwa kutumia waundaji wa magari wazawa, hivyo kuondoa kero ya muda mrefu na kuwalinda watumishi kutokana na madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi.
Nyingine ni kutengeneza sera na miongozo mbalimbali ya kiutawala amabayo ni muhimu kwa uendeshaji wa taasisi yoyote. 

Mipango, sera na miongozo isyopungua 12 iliandaliwa ikiwemo Communication and Marketing Policy and strategy ambapo hadi kufikia Juni 30, 2022 imeidhinishwa na inatumika,Research policy and guidelines hadi kufikia Juni 30, 2022 imeidhinishwa na inatumika.

Nyingine ni Anti-corruption policy,Health Policy,Risk Management Policy,Resource Mobilization Policy, Training Policy and Program, Human resource Plan and Succession Planning, Client Service Charter na  Scheme of Service (Muundo wa Utumishi 2020) ambapo hadi kufikia Juni 30, 2022 zimeidhinishwa na zinatumika.

Mambo mengine ni kupitia na kupendekeza maboresho ya sheria iliyoanzisha TAEC na kuidhinishwa na Bodi. Hii ni kutokana na mahitaji ya sasa yamebadilika kulingana pale mwanzo. 

Pia mapungufu mbalimbali kama yale ya kushindwa kusimamia vema usalama wa mionzi kwa sababu ya mapungufu ya sheria yamezingatiwa. 
Kuongoza katika kupitia na kuboresha kanuni saba zilizopitishwa na Bodi. Hii ni mhimu sana ili kuweza kuleta matokeo chanya ya utendaji wa kazi. 

Kanuni hizi zitaongeza ufanishi na matokeo ya kazi zikisha sainiwa na Mh. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia. Kwa sasa michakato unaendelea katika mamlaka husika. Katika hizo kanuni moja imekwisha kusainiwa na kutangazwa katika Gazeti la Serikali.

Pia kuongeza kasi na ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia inayofadhiliwa na Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA). 

Hii imefanyika kwa kuchukua hatua mbalimbali. Kwanza kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za miradi inayofadhiliwa na IAEA. 

Pia kurejesha mahusiano na mawasiliano mazuri na IAEA umesababisha kuinuka kwa utendaji katika miradi husika. Matokeo yake tukawa wenyeji wa mkutano wa waratibu wa kitaifa kutoka nchi 45 za Afrika mwezi Marchi 2019 uliofanyika Arusha. 

Kabla ya Aprili 2018, utendaji wa miradi ulishuka hadi kufikia 36%. Kwa muda mfupi wa kuwepo kwenye uongozi kasi ya utekelezaji ilipanda mpaka 91% (implementation rate).

Aidha, kuongezeka kwa shughuli za kujitangaza kwa asilimia 578.09. Hii imefanyika kwa njia mbalimbali. Njia moja wapo ni pamoja na kuimarisha kitengo cha mawasiliano. 
Hii inaendana na kuteua mkuu wa kitengo na kuweka kamati inayo ratibu kazi zake ambayo hukutana kila wiki. Tume imekua ikitumia mbinu mbalimbali kujitangaza vikiwemo vipindi ya TV na Redio pamoja na mitandao ya jamii na njia mbalimbali ili kuwafikia wananchi (Elimu kwa Umma) na kuwaeleza shughuli za tume.

Kuongeza tengeo la fedha za utafiti. 

Moja ya nguzo kuu ya taasisi ya sayansi ni kutekeleza majukuu yake maku na kufanya tafiti. Tangu kuingia kwa Prof. Busagala (2018-2022), tengeo la fedha za utafiti limeongezeka toka bajeti ya sufuri hadi takribani shilingi million 450 kwa mwaka. 

Matokeo chanya ya kutenga bajeti ni pamoja na kuwajengea uwezo wanasayansi katika kubobea kwenye sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Kusaidia kupanda kwa madaraja na mishahara kwa wafanyakazi kwani kigezo cha watafiti ni kupanda kwa machapisho.

Kuongezeka kwa idadi ya machapisho. Hadi kufikia mwishoni mwa 2021/2022, TAEC ilikuwa na inauwezo wa kutoa machapisho kwa wastani 7 kwa mwaka ukilinganisha na machapisho 11 ambayo yalipatikana tangu 1983 kufikia 2018. 
Machapisho haya ni muhimu hasa kukuza sayansi ya Nyuklia nchini na kuifanya iwe ya manufaa zaidi. Pia hutumika kuitangaza TAEC katika ulimengu wa ssyansi ya nyuklia.

Kuongezeka ununuzi wa vifaa vya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia. Vifaa vya kisayansi ni nguzo muhimu katika tafiti, usimamizi na uendelezaji wa Teknolojia ya Nyuklia. 

Jitihada za wazi za uongozi wa MM zimehakikisha kwamba vifaa vya kisayansi vinanunuliwa na kutumika katika maabara za TAEC makao makuu na kwenye ofisi za kanda na mipakani na hivyo kuongeza wigo wa usalama na udhibiti wa mionzi. 

Kwa sasa bajeti ya ununuzi wa vifaa vya kisayansi ni shilingi milioni 475 kwa mwaka. Pamoja na vifaa vingine vingi TAEC imenunua vifaa vya kukagua vyakula vyenye thamani ya 43,941€ kwa kila kimoja, kupeleka na hatimae kutengeneza kifaa cha maabara nje ya nchi ambayo gharama yake ni 26,617€ pamoja na kifaa cha alfa chenye gharama ya 32,867€. 

Pamoja na hayo wadau wa maendeleo wakati wa MM waliipatia TAEC jumla ya vifaa vyenye thamani ya fedha za kitanzani bilioni 6 ilipatikana kwa ajili ya maabara za gama, alfa beta. Vifaa hivyo ni kigunduzi cha mionzi cha ‘Sodium Iodeide, kigunduzi cha Hyper Pure germanium na vifaa vingine vya kutayarisha sampuli.

Kuongeza na kusimamia udhibiti matumizi salama ya mionzi ili kuepuka madhara yake. Madhara ya kutokagua ni kusababisha matumizi holela ya vyanzo vya mionzi. 

Kumekuwa na ongezeko la kaguzi kila mwaka. Hadi kufikia mwaka 2021/2022 jumla kaguzi 642 kwa mwaka zilifanyika ukilinganisha na kaguzi 244 kwa mwaka 2016/2017. Hili ni ongezeko la asilimia 174. Kaguzi hizi ni nyingi kuliko viwango vya kimataifa vinavyotaka.

Katika kudhibiti matumizi salama ya mionzi, uongozi ulifanikiwa kuongeza idadi ya wale wanaopewa lesseni kwa asilimia 102 yaani kutoka lesseni 297 kwa 2016/2017 hadi wastani wa 600 kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 

Sababu kubwa ya matokeo haya ni ongezeko la juhudi za udhibiti ikiwemo kufanya kaguzi za mara kwa mara, kufungua ofisi na kutumia mifumo ya TEHAMA.

Kuwasogezea wananchi huduma kwa kuanzisha, na kufungua na kuwezesha ofisi ishirini (24) zaidi za mipakani, mikoani na kanda nne ili kusogeza huduma kwa wananchi hivyo kuinua shughuli za kiuchumi za wananchi. 

Ofisi hizo ni ongezeko la asimilimia 200 ambapo linafanya TAEC kuwa na ofisi thelathini na tatu (40) nchi nzima. Kwa ujumla, ofisi hizo zipo sehemu mblalimbali ya nchi ikiwa ni pamoja na Abeid Amani Karume International Airport (Zanzibar), Arusha, Bagamoyo, Bukoba (Kagera), Dar es salaam, Dodoma, Horohoro (Tanga), Holili (kilimanjaro), Kibirizi (Kigoma), Kabanga (Ngara), Kabwe Port (Rukwa), Kasumulu, Katavi, Kigoma, Kilambo (Mtwara), 

Kilimanjaro International Airport (KIA), Kilwa-masoko (Lindi), Manyovu, Mbeya, Mbweni, Morogoro, Mtambaswala (Mtwara), Mtwara, Mutukula (Kagera), Mwanza, Mwanza Airport, Mwanza South, Namanga (Arusha), Pemba, Sirari (Mara), Rusumo, Tabora, Tanga, Tarakea (Kilimanjaro), Tunduma, Zanzibar na Zanzibar One Stop Centre. Jijini Dar es Salaam pia kulifunguliwa ofisi ndogongo 24 ili kuwahudumia wananchi kwa ukaribu.
Kuongeza vifaa kwenye maabara za mipakani na kanda. Ofisi 36 zimepewa vifaa kwa ajili ya kufanya upimaji wa awali. Hii ni sambamba na kuwekewa samani na vitendea kazi vingine. Zingine ndo zimefunguliwa hivi karibuni mchakato wa kutoa vifaa unaendelea. 

Katika utekelezaji wa Sheria ya Nguvu za Atomu Na. 7 ya 2003, kwa mara ya kwanza MM amesimamia usajili wa wataalam wa mionzi 656 wenye sifa za kutoa huduma ya mionzi ya ayanaizi kwa watu. 

Pia kwa mara ya kwanza tulisajili wataalam 37 wa kutengeneza na kukarabati vifaa vya nyukilia. Jambo hili lilikuwa halifanyiki kwa kipindi cha nyuma, ambapo lipo kwa mujibu wa sheria ya TAEC. 

Kuongoza uundaji wa Miongozo kumi na saba (17) ya Udhibiti wa Usalama wa Matumizi ya Vyanzo vya Mionzi katika matumizi mbalimbali ya mionzi.

Kuongoza TAEC katika ununuzi wa vifaa 110 vya udhibiti wa matumizi salama ya mionzi kama vile mashine ya MiniTrace, vifaa vya kudhibiti ubora wa Raye Safe, vifaa vya kugundua mionzi ili vitumike kuthibiti hali ya usalama wa mionzi kwenye vituo vya mionzi na mipaka.

Kubuni na kuanza kutekeleza miradi ya matumizi salama na ya amani ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia ambayo itawezesha TAEC kutimiza majukumu yake kwa manufaa zaidi. 

Mipango iliyopo 

TAEC imepanga kuleta mchango mkubwa zaidi kupitia Sayansi na Teknolojia ya Nyukilia katika maendeleo ya Taifa hasa katika sekta ya kilimo, elimu, viwanda na afya. 

Pamoja na kuwa na mipango mingi kwenye mpango mkakati, kuna miradi ambayo inafaida kubwa na imepewa kipaumbele kwa taifa ambayo ikitekelezwa italeta matokeo chanya kwa haraka zaidi katika nchi. Miradi hiyo ni pamoja na:

Kuendelea kuwasogezea wananchi huduma kwa kuimarisha maabara za mipakani na kanda ikiwa ni pamoja na kusimika vifaa na mitambo husika. 

Hii ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa maabara za kanda zilizo kwenye hatua mbalimbali na kuanza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Mbeya na Mtwara. 

Ujenzi wa maabara za kanda utawezesha kusogeza huduma kwa wananchi. Kama atapata ridhaa ya kuteuliwa tena utekelezaji wa jambo hili utafanyika kwa ufanisi na weledi mkubwa.

Mionzi salama

Mradi wa kuanzisha matumizi salama ya mionzi katika kuhifadhi mazao mbalimbali ikiwemo matunda, bidhaa za viwandani na hospitalini (multipurpose irradiator yaani kinunurisho jumuishi) ili kuyapa thamani na kuongeza usafirishaji nje ya nchi. 

Hivi sasa matunda na mazao mbalimbali hupelekwa nje ya nchi kibiashara, lakini upotevu unakadiriwa kufikia hadi asilimia 60. 

Pia mboga mboga na matunda huharibika kirahisi. Mradi huu ukiwepo utakuwa faida kubwa kwa utoaji elimu kwenye sayansi na teknolojia ya nyuklia. 

Aidha vifaa tiba na viwandani mbalimbali zinaweza kufanyiwa usalama (sterilization). Ujenzi wa miundombinu umekwisha kuanza. Utekelezaji wa kumalizia jambo hili unahitaji kiongozi makini kama Prof. Busagala.

Kinu cha utafiti

Mradi wa kinu cha utafiti cha nyuklia (Nuclear Research Reactor). Mradi huu ni muhimu sana kwa ajili ya utafiti, kufundishia na kuweka mazingira ya kuwa na viwanda vya madawa ya kutibu saratani (radio-pharmaceautical industries). 

Vinu vingi vya nyuklia duniani vya namna hii hutumika kwa utafiti na mafunzo, majaribio ya ubora wa vifaa, au utengenezaji wa isotopu za dawa. 

Kwa sasa Tanzania inatumia gharama kubwa kuagiza madawa ya namna hii. Na vyuo vikuu havina sehemu ya kufundishia wanafunzi. Zaidi baadhi ya tafiti haziwezi kufanyika kwa sababu ya kutokuwa na kinu cha utafiti cha nyuklia.

Vile vile, TAEC imedhamiria kuimarisha usalama wa mionzi nchini kwa kuanzisha chuo cha mafunzo ya sayansi na teknolojia ya nyuklia ikiwa pamoja na mafunzo ya muda mfupi mfupi. Maandalizi cha kuwa na chuo cha mafunzo tayari yanaendelea. Prof. Busagala atafaa kumalizia kazi hii.

Mipango mingine ni kuendelea kuboresha udhibiti wa matumizi salama ya mionzi na miundombinu ya teknolojia ya nyuklia.

Kuendelea kuweka na kuboresha kanuni na sheria ili kuwaweka watanzania salama zaidi dhidi ya madhara ya mionzi na teknolojia ya nyuklia. 
Pia kuendelea kujaza nafasi za watumishi zilizo wazi na kuwapa maslahi yao ili watumike kwa ufanisi zaidi, kufanya na kuendeleza miradi ya utengenezaji wa mbegu mbalimbali ili kuinua kilimo nchini na kuanzisha kituo cha utafiti cha dawa ya nyuklia.
Maombi

TAEC inawaomba wadau wote waendelee kuunga mkono juhudi za uongozi uliopo ili kuwezesha kupata mafanikio mazuri zaidi. 

Hata hivyo, TAEC inahitaji kuwezeshwa kwenye suala la watumishi na suala ya kifedha kwenye miradi iliyobuniwa ili kuweza kuweka msukumo kwenye Tanzania ya viwanda, hivyo kuboresha zaidi huduma za matibabu haya yale ya saratani.Kazi ilivyoanza inapaswa kuongeza juhudi zaidi ili kuendelea vema zaidi. 

Post a Comment

0 Comments