TANZIA:Mchezaji Iddy Moby Mfaume wa Mtibwa Sugar afariki

NA MWANDISHI WETU

BEKI wa Mtibwa Sugar, Iddy Moby Mfaume amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma. 

Kwa mujibu wa daktari wa Hospitali ya Kampuni ya Mtibwa Sugar, Khalid Sabuni, Mobby alipata tatizo la kiafya jana (Machi 4, 2023) mkoani Morogoro wakati akiwa katika mazoezi binafsi ya kutembea (road work) kuelekea mchezo wao wa ASFC dhidi ya KMC. 
….akiwa anaelekea uwanjani, alianza kupata tatizo la kuumwa kichwa, kisha alisikia kizunguzungu na kutaka kuanguka lakini alipiga magoti,”amesema Dkt. Sabuni wakati akithibitisha kifo hicho. 

Dkt. Sabuni amesema, Mobby alipelekwa katika hospitali hiyo ya kampuni, na kisha hospitali ya Bwagala kwa ajili ya matibabu zaidi lakini ilipofika usiku hali ilikuwa mbaya na hivyo kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma ambako umauti umemfika. 

..alifika Dodoma usiku lakini kufikia mchana wa leo akawa amefariki,a"Dkt. Sabuni. 

Iddy alisajiliwa Mtibwa Sugar msimu huu akitokea Ruvu Shooting lakini aliwahi pia kuzichezea timu za Geita Gold, Polisi Tanzania, na Mwadui FC kwa nyakati tofauti na pia aliwahi kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’. (Azamtv)

Post a Comment

0 Comments