TFF yamtangaza Adel Amrouche kuwa kocha mkuu Taifa Stars

NA DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Adel Amrouche (58) kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars.

Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika baada ya kufundisha klabu na timu za taifa katika ukanda Kusini, Mashariki, Kati na Kaskazini.
 
Amewahi kuwa Kocha Bora wa Afrika Mashariki mwaka 2013 wakati akiinoa na kuipa Kenya, Harambee Stars ubingwa wa Cecafa Challenge na kabla alifika nusu fainali mara mbili akiwa na Burundi.
 
Akiwa na Harambee Stars aliweka rekodi ya kucheza michezo 20 bila kupoteza.
Kocha Amrouche amewahi pia kuzinoa timu za taifa za Equatorial Guinea, Botswana, Libya na Yemen kwa nyakati tofauti.
 
Akiinoa DC Motema Pembe aliiwezesha kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho akiwa ameipa mara mbili ubingwa wa DR Congo na DRC Super Cup.
 
Uzoefu mwingine kwa klabu, amezifundisha RC Kouba, USM Alger, alizowahi kuzichezea na MC Algiers, zote za Algeria. Aidha, Kocha Adel ni mkufunzi wa walimu wa Pro Licence wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) akizalisha makocha wengi bora barani Afrika na ana uzoefu mkubwa katika soka la vijana, kazi aliyoifanya kwa zaidi ya miaka 10 nchini Algeria na Ubelgiji.
 
Kocha Amrouche anayezungumza lugha za Kiarabu, Kifaransa, Kingereza na Kiswahili, kwa nyakati tofauti, amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Michezo katika klabu za Ubelgiji na Ukraine.
 
Kocha mwenye Uefa Pro Licence na Shahada ya Uzamili katika kuwasoma watu na Utimamu (Mas- ters in Ergonomics in Physical Activity) Amrouche amekuwa akifanya kazi za ukufunzi pia kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kuzalisha walimu wa soka. 
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, katika wakati wote wa Mkataba wake Amrouche atalipwa mshahara na Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news