India kuipiku China kwa idadi ya watu duniani mwaka huu

NA DIRAMAKINI

TAKWIMU za idadi ya watu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kupitia "Ripoti ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani, 2023" inakadiria idadi ya watu wa India kuwa milioni 1,428.6 au bilioni 1.4286 dhidi ya bilioni 1.4257 ya China.

Ongezeko la kila mwaka la idadi ya watu nchini India limefikia wastani wa asilimia 1.2 tangu 2011. UNFPA imefafanua kuwa, India iko njiani kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani, ikiipita China ikiwa na takribani watu milioni tatu zaidi katikati ya mwaka huu.

Kwa mujibu wa Reuters, kulingana na takwimu za hivi karibuni, Marekani inakadiriwa kuwa na watu milioni 340 kufikia Februari 2023.

Aidha, wakati India inatarajiwa kuipita China kwa idadi ya watu hivi karibuni, ripoti ya hivi punde kutoka shirika hilo la kimataifa haikutaja tarehe ya lini mabadiliko hayo yatafanyika.

Kulingana na maafisa wa Umoja wa Mataifa, haikuwezekana kutaja tarehe kwa sababu ya kutokuwa na uhakika juu ya takwimu kutoka India na China,kwani sensa ya mwisho ya India ilifanyika mwaka 2011 na iliyofuata mwaka 2021 matokeo yamecheleweshwa kwa sababu ya Uviko-19.

Hata kama India na China zitachangia zaidi ya theluthi moja ya makadirio ya idadi ya watu duniani ya bilioni 8.045, ukuaji wa idadi ya watu katika mataifa makubwa ya Asia umekuwa ukipungua, kwa kasi zaidi nchini China kuliko India.

Mwaka jana, idadi ya watu wa China ilipungua kwa mara ya kwanza katika miongo sita. Wakati huo huo, ongezeko la kila mwaka la idadi ya watu nchini India limefikia wastani wa asilimia 1.2 tangu 2011, ikilinganishwa na asilimia 1.7 katika miaka 10 iliyopita, kulingana na takwimu za serikali.

"Matokeo ya uchunguzi wa India yanaonyesha kuwa wasiwasi wa idadi ya watu umeingia katika sehemu kubwa ya umma," Andrea Wojnar, Mwakilishi wa UNFPA India, aliieleza Reuters.

"Hata hivyo, idadi ya watu haipaswi kusababisha wasiwasi au kusababisha hofu. Badala yake, zinapaswa kuonekana kama ishara ya maendeleo, na matarajio ikiwa haki za mtu binafsi na chaguzi zinazingatiwa,"alisema.(Reuters/Businesstoday)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news