Kiongozi wa Mbio za Mwenge awapa neno wazazi kuwaokoa watoto dhidhi ya dawa za kulevya nchini

NA DIRAMAKINI

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim amewasihi wazazi kudumisha malezi bora kwa watoto wao ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kupoteza nguvu kazi ya Taifa. 

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ili kushirikiana kwa pamoja kumaliza tatizo la dawa za kulevya Nchini. 
Kaim ameyasema hayo tarehe 03 Aprili 2023 alipotembelea banda la Mamlaka katika Maonesho ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge yaliyofanyika viwanja vya Sabasaba Manispaa ya Mtwara, ambapo Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ilitumia nafasi hiyo kutoa elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news