LATRA yatoa onyo vitendo vya ukiukaji wa maadili usafiri wa umma nchini

NA FATMA JALALA 

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeonya uwepo wa vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya Kitanzania kufuatia ongezeko hilo katika vyombo vya usafiri wa Umma nchini ikiwemo mabasi ya Wanafunzi.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu Suluo amesema, hali hiyo inatokana na wamiliki wa vyombo hivyo kutokuwa na wasimamizi madhubuti na weledi wa Kanuni za Usafiri wa Umma za Mwaka 2020.

"Kumekuwa na matukio ya kuwafanyia vitendo vya kikatili wanafunzi hasa wa kike kwenye mabasi ya Shule, na zipo taarifa za wanafunzi hawa kunajisiwa.Jambo hili halivumiliki na halikubaliki kwa ustaarabu wetu na umma huu wa Watanzania,"amesema Suluo.

Aidha, ameongeza kuwa, kwa sasa wameelekeza, shule zote kuwasilisha orodha ya mabasi yanayotoa huduma kwa shule husika na majina ya madereva, namba za leseni na NIDA. 
"Aidha, kila shule iwasilishe orodha ya wahudumu wa mabasi hayo (matroni na patroni) na namba zao za NIDA. LATRA kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inafanya mapitio ya Kanuni za Usafiri wa Umma ili kuongeza vigezo vya udhibiti wa mabasi ya shule,"amesema Suluo. 

Suluo amebainisha kuwa, LATRA imekuwa ikitoa matamko kadhaa kukumbusha mazuio ya kikanuni ikiwemo kufanya biashara, mahubiri ya dini na kuweka picha za video na miziki isiyo na maadili ya Kitanzania katika vyombo vya usafiri wa umma.
"Nakumbusha tena na ninasisitiza kila mmiliki azingatie kanuni hizo. Mkazo wangu ni kwenye video na miziki isiyo na maadili kwenye mabasi.Hapa tutashirikiana na Baraza la Filamu Tanzania na tutachukua hatua stahiki. 

"Kwa sasa kila mtoa huduma aanze kutathmini video na miziki inayopigwa kwenye magari yake endapo akikaa na mwanae, mzazi wake anaweza kuziangalia au kuzisikiliza? amehoji Suluo. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news