NABII MKUU KUONGOZA IBADA YA KUZALIWA UPYA MAENEO YOTE

NA BEATRICE MAINA

NABII Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie kesho anatarajia kuongoza ibada ya kuzaliwa upya maeneo yote ambayo itafuatiwa na sherehe kubwa ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake. 
Ibada hiyo itafanyika katika nyumba ya matamko Ngurumo ya Upako Kisongo jijini Arusha kuanzia majira ya saa sita mchana na kuendelea.

Aidha, watu wote wametakiwa kuja na sadaka maalum ya kujiambatanisha na matamko ya kinabii atakayotamka Katika ibada hiyo.

Pia baada ya ibada kutakuwa na sherehe kubwa ya kukumbuka kuzaliwa kwa mtu wa Mungu Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie ambapo watu watakula,kunywa na kucheza.

Ibada hiyo pia itahudhiriwa na wageni kutoka ndani na nje ya nchi na pia watu wamejiandaa kutoa zawadi kwa Nabii Mkuu kwa kuwavusha katika maeneo mbalimbali maishani.

Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie alizaliwa April 25 mkoani Singida na amekuwa Mtumishi wa tofauti kwani wakati wote wamedumu kuwasaidia watu mitaji, magari,Bajaji,pikipiki na amewafungua watu wengi kutoka katika vifungo mbalimbali na kuwatoa kwenye mateso na umaskini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news