Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi katika sala ya Eid El Fitr

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia kazi zake Zanzibar,Mhe.Said Salim Al Sinawi, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Eid El Fitr iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya ”B” Unguja jijini Zanzibar leo Aprili 22, 2023 na kushoto kwake ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mussa Mahmoud Wadi.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh. Saleh Omar Kabi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Eid El Fitr iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya ”B” Unguja jijini Zanzibar leo na Kushoto kwake ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mussa Mahmoud Wadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais mstaafu wa Zanzibar, Alhaj Dkt.Amani Abeid Karume baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Eid El Fitr iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo ni baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Othman Hassan Ngwali akisoma dua baada ya kumalizika kwa sala ya Eid El Fitr iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jijini Zanzibar iliyofanyika leo, kushoto kwake ni viongozi wa dini na Mabalozi Wadogo wanaofanyia kazi zao Zanzibar wakishiriki kuitikia dua.
Baadhi ya Mabalozi Wagodo wanaofanyia kazi zao Zanzibar,viongozi wa dini na wananchi wakishiriki katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid El Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo.
Rsid wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akishiriki kuitikia dua ikisoma na Hatibu Sheikh Ally Abdurahaman Al Hilaal (hayupo pichani) baada ya hotuba ya Sala ya Eid El Fitr iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo, na kushoto kwa Rais ni Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh. Khalid Ali Mfaume na kulia kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Sheikh Ally Abdulrahaman Al Hilaal kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar akisoma hotuba ya Sala ya Eid El Fitr iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jijini Zanzibarleo baada ya Waumini wa Dini ya Kiislam kumaliza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news