RAIS DKT.MWINYI:NINA MATARAJIO MAKUBWA MAPENDEKEZO YA TUME YA MABORESHO YA TAASISI ZA HAKI JINAI TANZANIA

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kuunda Tume ya Maboresho ya Mifumo ya Taasisi za Haki jinai Tanzania kuleta tija kiutendaji kwa mifumo ya hiyo kwa mahitaji ya sasa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Tume ya Kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai,ulipofika Ikulu jijini Zanzibar leo kujitambulisha,chini ya Mwenyekiti wake Jaji Mkuu Mstaafu Mhe.Mohamed Chande Othman (wa tano kulia).(Picha na Ikulu).

Ameyasema hayo alipokutana na Tume ya Maboresho ya Mifumo ya Taasisi za Haki jinai Tanzania inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande.

Tume hiyo iliteuliwa na kuzinduliwa na Rais Dkt.Samia tarehe 30 Januari,2023 kutathmini na kuangalia maboresho ya mifumo ya haki jinai Tanzania. 

Aidha, Dkt.Mwinyi amesema ana matarajio makubwa ya mapendekezo kupitia ripoti ya tume hiyo ambayo itawasilishwa kwa Rais Dkt. Samia na kuonyesha marekebisho yanayohitajika katika mfumo mzima wa kimuundo wa taasisi za haki jinai kwa kuleta ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa utoaji haki kiufanisi zaidi na manufaa kwa Serikali zote mbili. 

Naye Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande amesema tume hiyo itazungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi, asasi za kiraia na kiserikali, pamoja na taasisi zinazoshughulikia haki jinai Jeshi la Polisi, Chuo cha Mafunzo, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Zanzibar, Uhamiaji, Mahakama na nyinginezo. Pia watazuru Mikoa ya Unguja na Pemba kwa siku nne kukutana na makundi hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news