Rais Dkt.Mwinyi:Tumejikita zaidi katika teknolojia kuboresha Sekta ya Utalii

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imejikiza zaidi kwenye teknolojia ya kisasa ili kuboresha sekta ya utalii kwa kuimarisha miundominu ya kisasa ya utoaji huduma bora kupitia viwanja vya ndege vya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, alipofika Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu. (Picha na Ikulu).

Lengo likiwa ni kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbambali ya duniani wanaoitembelea Zanzibar ili wakirudi kwao wawe mabalozi wazuri wa kusimulia mazuri yanayopatikana kwenye visiwa vya Unguja na Pemba na Tanzaia kwa ujumla.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, Ikulu Zanzibar aliyefika kujitambulisha.

Mheshimiwa Dkt. Mwinyi, alimueleza balozi huyo kwamba Zanzibar utalii ndio sekta mama ya uchumi ambao inahusisha na sekta nyingine za uwekezaji kupitia sera yake ya uchumi wa Buluu.

Rais Dkt.Mwinyi amesema, uhusiano uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania ikiwemo Zanzibar kumekuwa na urafiki mzuri baina yao kwani nchi imekuwa ikipokea watalii wengi kutoka huko.

Amesema, kupitia sekta ya utalii kumekuwa na safari za ndege za moja kwa moja kutoka Ubelgiji hadi Zanzibar na kumueleza balozi huyo uhusiano uliopo baina ya pande mbili hizo anaamini wataalii zaidi wataongezeka katika kuimarisha urafiki wao.

“Zanzibar tuna safari za ndege za moja kwa moja kutoka Ubegiji, hali hii pia imeongeza watalii wengi kutoka huko, tunaamini idadi itaongezeka zaidi kutokana uhusiano mzuri baina yetu,” alisifu, Dkt. Mwinyi.

Akizungumzia sekta ya Afya, Rais Dkt. aliueleza balozi huyo kuangalia uwezekano wa kuimarisha ushirikiano zaidi kwenye sekta hiyo hasa masuala ya TEHAMA ambako eneo hilo lina uhitaji zaidi ili kuongeza ujuzi na kubadilishana uzoefu kwa wafanyakazi na wahudumu wa fani hiyo kupitia Taasisi ya Karume ambayo vijana wengi huchukua fani ya Afya.

Pia Rais Dkt.Mwinyi alimueleza Balozi Huyghebaert ikiwa Ubelgiji ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) yenye miradi mingi ya maendeleo kuangalia zaidi fursa zilizopo kupitia ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania ikiwemo Zanzibar kunufaika na fursa zilizopo huko na uwezekano wa kuzifikia katika kuimarisha zaidi uhusino baina yao.

Kwa upande wake Bolozi Peter Huyghebaert, aliishurkuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kumpongera Rais Dkt. Mwinyi kwa juhudi zake za kuiletea maendeleo Zanzibar.

Amesema, urafiki wa diplomasia uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania ikiwemo Zanzibar anaamini utaendelea kuzaa matunda mazuri yatakayowanufaisha wananchi wa pande mbili hizo.

Amesema, Ubelgiji imekuwa ikishirikiana zaidi na Afika kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa sekta zote za taasisi za umma na binafsi.

Alimueleza Rais Dkt. Mwinyi kwamba hadi sasa Ubelgiji inaendeleza miradi mbalimbali kwenye kanda tano za Afrika, Tanznia ikiwa miongoni mwao kwa kuyafikia maeneo mengi hasa kwenye sekta mtandao ikiwemo kushirikina katika masuala ya Afya mtandao ambako Ubelgiji na Tanzania wanashirikiana kwenye matumizi ya teknolojia ya kisasa kuangalia uwezekano wa kunusuru vifo vya watoto kabla ya kuzaliwa na nyinginezo.

Pia Balozi huyo alimuahidi Dkt. Mwinyi kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuimarisha matumizi ya TEHAMA na teknolojia hasa kwenye sekta ya afya kwa kuimarisha huduma za Afya mtandao pamoja na kuangalia fursa zilizopo kupitia uchumi wa buluu jinsi ya kuwanufaisha wananchi wa pande mbili hizo katika kuendeleza uhusiano wa kirafiki uliopo baina yao.

Tanzania na Ubelgiji zimekua na uhusiano wa diplomasia na biashara tangu miaka ya 1980 ambapo kwa mara ya kwanza Ubelgiji ilifungua ubalozi wake Dar es Salaam mwaka huo na Tanzania ilifungua ubalozi wake mji mkuu wa nchi hiyo, Brussels ambako balozi wa Tanzania nchini humo ni Mhe. Jestas Abouk Nyamanga tangu mwaka 2019.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news