Rais Dkt.Ruto aahidi uwekezaji zaidi katika Sekta ya Maji

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Jamhuri ya Kenya imesema itaongeza uwekezaji katika miundombinu endelevu inayohusiana na maji nchini. 

Mheshimiwa Rais Dkt. William Ruto amesema, hatua hiyo inalenga kuiwezesha nchi kuwa na usalama wa maji.
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Maji wa Mavoko ambao umegharimu fedha za Kenya shilingi bilioni 2.7 huku akisisitiza jitihada hizo zitaokoa maisha na kuboresha afya za watu.

Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto amesema, mradi huo utahudumia zaidi ya watu 500,000 katika maeneo ya Mavoko, Athi River, Mlolongo na Syokimau huko Machakos.
Pia amesema, mradi huo utaongeza lita milioni 12 za ziada za maji kila siku kwa kaya. Rais Dkt.Ruto alibainisha kuwa, amejitolea kufanya kazi na viongozi wote, licha ya msimamo wao wa kisiasa, kuwawezesha Wakenya.

Kwa upande wake Gavana wa Machakos, Wavinya Ndeti aliipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa katika mradi wa maji.“Huu si wakati wa siasa, tuna masuala muhimu zaidi ya kushughulikia,”alisema Gavana huyo.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje, Mheshimiwa Alfred Mutua alisema, Serikali imejitolea kuwahudumia Wakenya kwa nguvu zote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news