Rais Dkt.Samia ashuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya uchimbaji madini

NA MWANDIHI WETU

MKURUGENZI wa Mtendaji wa Kampuni ya Evolution Energy Ltd Phil Hoskins inayotarajia kuanza mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe katika eneo la Chilalo wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi amesema anaamini mikataba iliyosainiwa leo Aprili 17, 2023 italeta maendeloa kwa pande zote mbili pamoja maendeleo ya baadae.
Aidha, Hoskins amesema mkataba uliosainiwa leo ni wa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Evolution Energy Ltd na ambayo itachangia maendela ya wilaya ya Ruangwa na Taifa kwa ujumla.

Pia, Hoskins amesema Kampuni ya Evolution Energy Ltd itaendelea kufanya tafiti katika mradi wa Chilalo kwa lengo la kuongeza Maisha ya mradi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Hoskins amesema jumla ya uwekezaji wa awali katika mradi wa Chilalo ni Dola za Marekani 100 ambapo mradi unatarajiwa kuajiri Zaidi ya watanzania 100 katika hatua ya ujenzi wa mradi huo.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya EcoGraf Ltd Andrew Spinks unaotarajiwa kuchimba madini ya Kinywe katika eneo la Epanko wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro amesema madini ya katika hatua ya awali kampuni hiyo imepanga kuwekeza jumla ya Dola za Marekani milioni 127.7 na kutoa gawio kwa serikali la asilimia 16 zisizofifishwa na kampuni hiyo kumiliki hisa za asilimia 84. 

Pia, Mwenyekiti wa Kampuni ya Peak Rare Earths Ltd Russel Scrimshaw inayotajia kuanza uchimbaji wa madini ya Rare Earth Element katika mradi wa Ngualla uliopo wilaya ya Songwe mkaoni Songwe amesema, Rare Earth ni madini muhimu na ni madini ya kimkakati ambayo yanatumikakutengeneza betri za magari ya umeme na matumizi mengine ya teknolojia.

Katika hatua nyingine, Scrimshaw amesema mradi wa Ngualla unatarajiwa kuajiri zaidi ya watanzania 300 katika kipindi cha awali cha ujenzi wa mradi ambapo ina jumla ya uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani 437 pamoja na thamani za mauzo ghafi yatakuwa kiasi cha shilingi bilioni 1,860

Tunaposhuhudia mkiataba ya miradi mbalimbali ya madini ikisainiwa ni kielelezo kwamba nchi imefunguka kiuchumi na sasa wawekezaji wanamiminika Tanzania kitu ambacho kinaonesha uongozi na, usimamizi na maelekezo ya Rais nchi katika Sekta ya Madini yanazingatiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news